Tanzania Yahodhi Mashindano ya Ngalawa (African Dinghy Championship)

Tanzania imefanikisha kuyahodhi mashindano ya Afrika ya ngalawa kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 yaliyofanyika mwezi Agosti, mwaka 2012 kwa mafanikio makubwa huku ikishuhudia mshindi wa jumla akitokea nchini Afrika Kusini. Mashindano hayo yalizinduliwa rasmi na Mh. Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Dr. Fenella Mukangara katika ufukwe wa Bahari ya Hindi, maeneo ya Yacht Club Masaki, jijini Dar Es Salaam. Mashindano haya yalishirikisha timu toka mataifa mbalimbali ya Afrika kama vile: Zimbabwe, Tunisia, Angola, Algeria, Afrika Kusini, Misri, Kenya na wenyeji Tanzania. Pia zilikuwapo timu waalikwa toka nchi ya Oman.

Na John Chalukulu – Afisa Michezo, Baraza la Michezo

20 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2012/12/17/tanzania-yahodhi-mashindano-ya-ngalawa-african-dinghy-championship/">
RSS