Uchaguzi wa Chama cha Mpira wa Wavu

Chama cha Mpira wa Wavu Tanzania (TAVA) kimefanya uchaguzi wake mkuu jijini Tanga tarehe 18 Mei 2013 katika hoteli ya mkonge. Uchaguzi huu ulisimamiwa na Baraza la Michezo la Taifa na ulifanyika ka kutumia rasimu ya katiba ya chama cha mpira wa wavu Tanzania baada ya makubaliano ya wajumbe wa mkutano mkuu wa chama cha mpira wa wavu Tanzania (TAVA). Mkutano mkuu wa uchaguzi ulihudhuriwa na wajumbe kutoka mikoa 14 ambayo ni:

 1. Tanga
 2. Pwani
 3. Mtwara
 4. Morogoro
 5. Tabora
 6. Ruvuma
 7. Rukwa
 8. Geita
 9. Mwanza
 10. Kilimanjaro
 11. Shinyanga
 12.  Dodoma
 13. Dar es salaam
 14. Mara- Hawakuruhusiwa kupiga kura kwa kukosa barua ya katibu Tawala Mkoa.

Viongozi waliochaguliwa:

Na. Jina Nafasi ya uongozi
1. Augustino Agapa Mwenyekiti
2. Muharam Muchume Makamu wa 1 wa Mwenyekiti Maendeleo na Mipango.
3. Goerge John Makamu wa 2 wa Mwenyekiti Fedha na Utawala.
4. Allen Alex Katibu Mkuu
5. Somo Kimwaga Mwenyekiti kamati ya Ufundi
6. Kokono David Mabula Mwenyekiti kamati ya wavu ufukweni
7. Nkane Nkane Ally Mwenyekiti kamati ya kuendeleza mikoa
8. Adolfina Hamis Mwenyekiti kamati ya maendeleo ya watoto.
9. Theonestina Nyarufunjo Mwenyekiti kamati ya maendeleo ya wanawake.
10. Siraju Mwasha Mwenyekiti kamati ya waamuzi
11. Amoni Sifaeli Mwenyekiti kamati ya kuendeleza mashule.
12. Emmanueli Majengo Mwenyekiti kamati ya Makocha

Nafasi ya katibu mkuu msaidizi ilikosa mgombea na itajazwa kulingana na matakwa ya katiba ya chama cha mpira wa wavu Tanzania.

Na Benson Chacha; Afisa Michezo; Baraza la Michezo

48 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2013/06/06/uchaguzi-wa-chama-cha-mpira-wa-wavu/">
RSS