TAARIFA KWA UMMA KUPITIA VYOMBO VYA HABARI

Sera ya Maendeleo ya Michezo na Sheria ya Baraza la Michezo la Taifa pamoja na Kanuni zake zinatengeneza mazingira ya kuendeleza huduma za Tiba na Kinga kwa Wanamichezo na mafunzo kwa Wataalamu wa tiba kwa Wanamichezo (Sports Medicine).

Katika juhudi za kutekeleza Sera na Sheria hizo Baraza la Michezo la Taifa kwa kushirikiana na Chama cha Wataalamu wa Tiba ya Wanamichezo Tanzania (TASMA), wameandaa mafunzo kwa Madaktari wa Michezo ambayo yatafanyika katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam mnamo tarehe 14 – 18 Julai, 2014.

Lengo la mafunzo haya ni kuwaongezea washiriki ufahamu na ujuzi zaidi ili waweze kumudu majukumu yao vizuri na kuchangia kikamilifu katika kuleta ushindi kwenye michezo na mashindano mbalimbali.  Pia kuongeza idadi ya wataalamu hao ili kuziba pengo kubwa lililopo kwenye Vilabu na Taasisi mbalimbali za michezo hapa nchini. Wataalamu hawa watasaidia sana kudhibiti matukio mbalimbali viwanjani vikiwamo vifo vya wanamichezo.

Washiriki wanaombwa kuchangia shilingi laki mbili (200,000) ili kufidia gharama za kuendesha mafunzo.  Malipo yafanyike kupitia Akaunti Na. 20401100013 Benki  yoyote ya NMB. Mawasiliano yeyote yanayohusiana na ushiriki yatumwe kwa Katibu Mkuu Baraza la Michezo au Simu namba 022111943 au 0716661088.

Vilabu, Taasisi na Wataalamu binafsi wanaombwa  kuhudhuria mafunzo haya muhimu kwa ajili ya maendeleo ya michezo nchini.

“Pamoja tunaweza”

Nashukuru sana kwa ushirikiano wenu.

Imetolewa na:

Benson J. Chacha

KNY: KATIBU MKUU

76 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2014/07/02/taarifa-kwa-umma-kupitia-vyombo-vya-habari/">
RSS