TOPLAND KINONDONI MABINGWA SAFARI POOL TAIFA 2014

Baadhi ya wachezaji wa klabu ya Topland wa mkoa wa kimichezo wa Kinondoni wakishangilia na kikombe pamoja na pesa Taslimu Tsh. 5,000 000/= mara baada ya kuibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya Safari Pool Taifa yaliyomalizika mwishoni mwa wiki Mkoani Kilimanjaro.

 

 

 

 

 

 

 

Klabu ya Topland ya Mkoa wa Kimichezo wa Kinondoni yenye makazi Magomeni jijini Dar es Slaaam imefanikiwa kutetea ubingwa wake wa fainali za mashindano ya Safari Pool Taifa yaliyomalizika mwishoni mwa wiki Mkoani Kilimanjaro kwa kuifunga timu ya Anatory ya Mkoani Morogoro 13-3.

Timu ya Topland kwa kutwaa ubingwa huo ilizawadiwa Kikombe, Medali za Dhahabu na Pesa Taslimu Tsh. 5,000,000/=, Mshindi wa Pili Timu ya Anatory ya Morogoro walizawadiwa Pesa Taslimu Tsh. 2,500 000/= pamoja na Medali za Fedha. Mshindi wa tatu katika fainali hizo ni Timu ya Mashujaa ya  Mkoa wa kimichezo wa Ilala, Dar es Salaam ambao walizawadiwa Pesa Taslimu Shilingi 1,250,000/=  na Medali za Shaba. Washindi wanne ni Timu ya Mboya ya Mkoani Kilimanjaro ambao ndio walikuwa Wenyeji wa Mashindano haya mwaka huu, ambao walizawadiwa Pesa Taslimu Shilingi  750,000/=.

Upande wa mchezaji mmoja mmoja Wanaume, Mussa Mkwega kutoka klabu ya Anatory ya Mkoa wa Morogoro alitwaa ubingwa kwa kumfunga Innocent Sammy kutoka Mkoa wa kimichezo wa Temeke 5-4 na hivyo Mussa Mkwega kuzawadiwa fedha Taslimu Tsh. 500,000/=, Medali ya Dhahabu pamoja na Ngao. Mshindi wa pili Innocent Sammy alizawadiwa fedha Taslimu Tsh.  250,000/= pamoja na Medali ya Fedha.

Upande wa mchezaji mmoja mmoja wanawake, Neema Hamis kutoka Mkoa wa Tanga alitwaa ubingwa kwa kumfunga  Sada Tulla kutoka Shinyanga na hivyo kuzawadiwa pesa taslimu Tsh. 350,000/= pamoja na Medali ya Dhahabu wakati  Sada Tullah yeye kwa kukamata nafasi ya pili alizawadiwa pesa taslimu  Tsh. 200,000/=

Akikabidhi zawadi hizo Naibu Waziri wa Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia aliipongeza Kampuni ya Bia Tanzania kupitia bia yake ya afari Lager kwa kudhamini mashindano ya Pool Taifa na aliwaomba waendelee kufadhili kwani mpaka sasa ni mchezo pekee ulioiletea sifa Nchi kupia fainali za Afrika ambapo Mtanzania Patrick Nyangusi anashikilia Ubingwa wa Afrika.

Naibu Waziri Nkamia aliwataka pia Chama cha Pool Taifa(TAPA) kutumia vyema fursa ya TBL kwa manufaa ya kuendeleza mchezo huo nchini na Kimataifa na kwa jinsi hiyo aliwapa siku 60 wawe wameshafanya uchaguzi na kupata viongozi wa kuchaguliwa kikatiba na wa muda tangu chama hicho kianzishwa kama ilivyo sasa.

Mwisho Waziri Nkamia aliwatakia safari njema wanamichezo wote kurejea majumbani salama na kuwaomba walichokipata kwa Safari Lager kama zawadi wakakitumie vyema kwa maendeleo yao

Nahodha wa timu Topland ya Mkoa wa kimichezo wa Kinondoni, Patrick Nyangusi akishangilia na kikombe mara baada ya kuibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya Safari Pool Taifa yaliyomalizika mwishoni mwa wiki Mkoani Kilimanjaro.
Nahodha wa timu Topland ya Mkoa wa kimichezo wa Kinondoni, Patrick Nyangusi akishangilia na kikombe mara baada ya kuibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya Safari Pool Taifa yaliyomalizika mwishoni mwa wiki Mkoani Kilimanjaro.

21 total views, 2 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2014/09/16/topland-kinondoni-mabingwa-safari-pool-taifa-2014/">
RSS