MABADILIKO YA RATIBA SHIMIWI 2014

Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) linatoa taarifa kwa vilabu wanachama, wadau wa michezo kuwa michezo inayowakutanisha watumishi wa serikali (SHIMIWI)- 2014 ambayo ilipangwa kufanyika Mjini Dodoma Kuanzia tarehe 27 Septemba hadi 11 Oktoba, 2014, michezo hiyo sasa itafanyika mkoani Morogoro katika tarehe zilizotajwa hapo juu. Shirikisho limefikia uamuzi huu baada ya kuona kuwa Mkoa wa Dodoma unakabiliwa na shughuli nyingi za Kiserikali kwa sasa. Shirikisho linaomba radhi kwa vilabu vyote vinavyoshirikimichezo hii kwa usumbufu uliotokea kwani tunaamini kuwa walishafanya maandalizi ya kutosha ya kupeleka timu zao katika Mkoa huo. aidha, tunaomba radhi kwa wadau wa michezo na wananchi wa mkoa wa Dodoma kwa mabadiliko hayo. Mwisho Shirikisho linatoa wito kwa wadau wa Michezo na wananchi wa Mkoa wa Morogoro kuwa tayari kuupokea ugeni huu ambao Mh. Mkuu wa Mkoa huo ameuridhia, pia tunawaomba wajitokeze kwa wingi viwanjani kushuhudia Michezo hii.

38 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2014/09/23/mabadiliko-ya-ratiba-shimiwi-2014/">
RSS