MASHINDANO YA MICHEZO YA SHIMIWI 2014 YAFUNGULIWA JIJINI MOROGORO

Shirikisho La Michezo Ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI)  yamefunguliwa rasmi jana tarehe 28/09/2014 katika uwanja wa Jamuhuri Morogoro. Wadhamini wa mashindano haya ya SHIMIWI ni Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma PSPF. 

Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Mhe. Celina O. Kombani katika  Uzinduzi wa michezo ya SHIMIWI  kwa mwaka 2014 Mjini Morogoro.  “Alisema, waajiri katika  Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala na Taasisi za Serikali   wanatakiwa kutenga Bajeti na kuweka utaratibu mzuri kwa watumishi kushiriki katika michezo ili kujenga afya, ukakamavu na kufahamina.

Pamoja na ufinyu wa bajeti na kazi nyingi Waajiri  inabidi wadumishe  Michezo sehemu za kazi, kwani michezo inaepusha  maradhi ya mara kwa mara hasa yanayosababishwa na kukithiri kwa uzito ‘alisema Mhe. Kombani.

Aidha, Mhe. Celina aliwasihi wanamichezo kuwa na mshikamano na  kushirikiana katika kipindi chote cha michezo.

Kabla ya Ufunguzi akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Morogoro, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro,  Bw. Noeli Kazimoto aliwataka washiriki wa SHIMIWI   kuzingatia Maadili ya Utumishi wa Umma hata kama wako nje ya sehemu zao za kazi.

“ Lazima tudumishe nidhamu kwa kuwa bado sisi ni Watumishi wa  Umma” alisema Kazimoto.

Akimkaribisha Mgeni Rasmi kufungua mashindano,  Mwenyekiti wa SHIMIWI  Bw. Daniel Mwalusamba alitoa shukrani kwa uongozi wa Mkoa wa Morogoro kutoa ushirikiano katika kufanikisha mashindano hayo.

Wakati huo huo, timu ya mpira wa miguu ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi  na timu ya mpira wa miguu ya Mkoa wa Arusha zilitoka bila ya kufungana katika mechi ya ufunguzi, huku timu ya netiboli ya Ikulu ikishinda kwa kete 62 dhidi ya timu ya netiboli ya Mkoa wa Morogoro iliyoambulia kete 10.

Kwa upande wa kamba timu ya Wanaume ya Ikulu ilishinda kwa pointi 2 baada ya kuiburuza Wizara ya Nje  na Ushirikiano wa Kimataifa walioambulia patupu,  huku timu ya kamba ya wanawake ya Wizara ya Uchukuzi ilishinda kwa pointi 1 dhidi ya timu ya Mkoa ya Iringa ilitoka bila ya pointi.

Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) huandaa mashindano haya kila mwaka ambayo huwakutanisha watumishi wa Serikali kwa lengo la kuleta ushirikiano, upendo na undugu.

Timu ya Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo
Timu ya Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo

Baadhi ya Wachezi wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo.  Aliyekaa kushoto ni Dkt Ngome, Bi. Husna, Abuu Kombo, Meneja wa timu Azizi Mwaruka na aliyekaa ni Hashimu Yusufu.
Baadhi ya Wachezi wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo. Aliyekaa kushoto ni Dkt Ngome, Bi. Husna, Abuu Kombo, Meneja wa timu Azizi Mwaruka na aliyekaa ni Hashimu Yusufu.
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh.Celina O. Kombani (Mb) akihutubia katika ufunguzi rasmi wa  mashindano ya michezo ya SHIMIWI mjini Morogoro.
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh.Celina O. Kombani (Mb) akihutubia katika ufunguzi rasmi wa mashindano ya michezo ya SHIMIWI mjini Morogoro.
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh.Celina O. Kombani akisalimiana na wanamichezo wanaoshiriki mashindano ya SHIMIWI mjini Morogoro,wakati wa ufunguzi wa michezo ya SHIMIWI.

76 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2014/09/29/mashindano-ya-michezo-ya-shimiwi-2014-yafunguliwa-jijini-morogoro/">
RSS