MCHEZO WA MPIRA WA MIGUU KUTUMIKA KUTOA ELIMU YA VVU/ UKIMWI

bandar mpira

Baraza la Michezo la Taifa, limesema kupitia mpango wa “Tackle Africa” litaendelea kutumia Stadi za Mchezo wa Mpira wa Miguu kutoa Elimu ya VVU/UKIMWI kwa jamii. Baraza litawatumia walimu wa michezo katika ngazi ya mikoa na Wilaya za Tanzania bara ambao watapewa mafunzo ya jinsi ya kutoa ujumbe na kuihusisha elimu ya VVU/UKIMWI  kwa kutumia stadi za  Mpira wa Miguu.

Akizungumza wakati wa mafunzo ya Makocha Elekezi yaliyofanyika katika Viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es salaam tarehe 15-24 Aprili, 2013, mratibu wa mradi huo, Baraza la Michezo la Taifa Bi Halima Bushiri alisema mafunzo hayo yanatolewa kwa kuanza na  walimu/makocha elekezi (20) kutoka mikoa minne ya Tanzania bara ambayo  ni Dar es saalam, Lindi, Pwani, na Morogoro.

“Lengo ni kuwafundisha walimu wanawake wa michezo wapatao 20 kutoka mikoa 4 ambapo kila mkoa utakuwa na walimu 4 waliopata mafunzo haya na hao walimu tunategemea watawafundisha walimu wenzao 30 katika mikoa yao, hivyo ni matumaini yetu kuwa baada ya mwaka mmoja tutakuwa na walimu wanawake 150 waliopata mafunzo haya ambao  wataweza kuelimisha vijana na jamii yetu kuhusu masuala ya VVU/UKIMWI kupitia stadi za mpira wa miguu.” Alisisitiza Halima.

Halima alifafanua kuwa mpango huo umejikita kutoa mafunzo hayo kwa walimu/makocha wanawake wa michezo kwa kuamini kuwa ukimuelimisha mwanamke ni rahisi kuielimisha jamii nzima. Aidha, michezo hujenga Afya na upendo na mwanamke anayo nafasi kubwa ya kuyatekeleza hayo  kupitia mpira wa miguu na hatimaye jamii nzima inaweza kuelimika juu ya VVU/UKIMWI kwa kupitia stadi za Mpira wa Miguu.

“Tunatarajia ifikapo Septemba, 2014, tutakuwa na Makocha Elekezi (20), na makocha walimu wanawake 150 wenye uwezo wa kufundisha Elimu ya VVU/UKIMWI kupitia stadi za Mpira wa Miguu  ambao watakuwa wanaweza kutoa elimu mashuleni na katika jamii kwa wastani wa wanafunzi na vijana 900 katika mikoa minne ambayo inashiriki mafunzo haya.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, mshiriki kutoka mkoani Lindi, Bi. Juliana Mokiwa  alibainisha kuwa mafunzo hayo yanatolewa kwa wakati muafaka kwa kuzingatia kuwa jamii yetu hasa vijana ndio wanoathirika sana na VVU/UKIMWI.

“Vijana wengi wamekuwa wakiaathirika na VVU/UKIMWI kutokana na kukosa elimu ya jinsi ya kujikinga na Ugonjwa huo lakini kupitia stadi za michezo hasa Mpira wa Miguu ambao unajulikana na unapendwa sana na jamii ya wengi  ni dhahiri kuwa tutaweza kutoa elimu sahihi,  kwa wakati sahihi kwa pamoja na kwa watu wengi na hatimaye kuwa na jamii iliyoelimika jinsi ya kujikinga na VVU/UKIMWI ”  alisema Mokiwa.

Programu ya “Tackle Africa” inaratibiwa na Baraza la  Michezo la Taifa na kufadhiliwa na Mradi  wa International Insipiration ambapo mafunzo yanatolewa na mtaalamu kutoka Uingereza. Lengo ni  kutoa Elimu ya VVU/UKIMWI kwa jamii  kupitia Stadi za Mchezo wa Mpira wa Miguu.

logo 

www.tackleafrica.org 

 

159 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by EmailO
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2014/10/07/mchezo-wa-mpira-wa-miguu-kutumika-kutoa-elimu-ya-vvu-ukimwi/">
RSS