TANZANIA KUANDAA FAINALI YA MCHEZO WA ALL AFRICA POOL CHAMPIONSHIP.

pool
mchezaji wa pool table na washabiki
Chama cha Mchezo wa POOL Tanzania kitakuwa mwenyeji wa mashindano “ALL AFRICA POOL CHAMPIONSHIP” ambayo yatafanyika kuanzia tarehe 16-18 Octoba, 2014, katika Ukumbi wa Budget Kunduchi JIJINI Dar es salaam.

Mashindano hayo yatafunguliwa tarehe 16 Octoba saa 12.00 jioni na yatafungwa tarehe 18 Octoba 2014 saa 1.00 usiku, Mashindano haya   yatashirikisha nchi (7) za Africa ambazo ni Africa ya Kusini, Lesotho, Zambia, Malawi, Kenya, Uganda na wenyeji wao Tanzania. Mashindano yatashirikisha Timu za Taifa za Wanawake na Wanaume na Mchezaji mmoja mmoja kwa Wanawake na Wanaume.

Zawadi zitatolewa kama ifuatavyo;

–         Timu bigwa wanaume USD 5,000.00 na medali za dhahabu

–         Mshindi wa pili USD 2,000.00 na medali za fedha

–         Mshindi wa tatu medali ya shaba

Mchezaji mmoja mmoja

–         Wanaume bigwa USD 2,000.00 na medali ya dhahabu

–         Mshindi wa pili USD 1,000.00 na medali ya fedha

–         Mshindi wa tatu medali ya shaba

–         Mwanamke bigwa USD 1,000.00 na medali dhahabu

–         Mshindi wa pili USD 500.00 na medali ya fedha

–         Mshindi wa tatu medali ya shaba

Mashindano yanadhaminiwa na kampuni ya bia Tanzania TBL kupitia bia ya Safari Lager.

 

pool 2
Meneja wa bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo (katikati akiongea na waandishi wa habari, na (kulia) ni Mwenyekiti wa Chama cha Mchezo wa Pool Table Isaac Togocho(wa kawanza kulia) na wa tatu kushoto ni Katibu wa chama cha Mchezo wa Pool Amos KafwingaTanzania (TAPA) .

pool
mchezaji wa pool table na washabiki

7 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2014/10/10/868/">
RSS