UBINGWA WA TAIFA MBIO ZA BAISKELI KUFANYIKA DAR

Michezo ya  ubingwa wa Taifa wa mbio za baiskeli  unatarajiwa kufanyika kwa siku mbili jijini Dar  es salaam badala ya Mbeya kama ilivyotangazwa  awali.

Akizungumza Dar es salaam jana, Katibu Mkuu wa Chama cha baiskeli Tanzania (CHABATA) John Machemba alisema kuwa michezo hiyo itafanyika Desemba 20 hadi 21,mwaka huu kutokana na kuongezeka kwa vipengele katika michezo ya kukaza mwendo.

Alisema mchezo mkubwa katika kumpata bingwa wa Taifa  itakuwa kilomita 160 kwa wanaume na kilomita 80 kwa wanawake na utafanyika kuifuata barabara ya Bagamoyo.

“Mchezo huu utatoa timu ya Taifa ambayo itakuwa na wachezaji 30, ambao 20 ni wanaume, 5 wanawake na 5 watakuwa ni chipukizi bila kujali jinsia zao” alisema Machemba.

Alisema hadi sasa wana wachezaji 120 na kwa upande wa Zanzibar imepanga kuwakilishwa na wachezaji 25 ambao bado wapo katika maandalizi ya mchezo wa mchujo.

Akizungumza juu ya Mkutano Mkuu wa kwanza kufanywa na CHABATA, Machemba alisema kuwa kutakuwa na mjadala wa wazi utakaofanyika siku mbili za mwanzo.

Alisema, wanaamini kuwa baada ya mkutano huo mchezo wa baiskeli utazaliwa upya na kuhusishwa kila kona ya nchi na chama kitachukua jukumu la kuuendeleza kwa kiwango kinachostahili.

 

8 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2014/10/15/ubingwa-wa-taifa-mbio-za-baiskeli-kufanyika-dar/">
RSS