Naibu Waziri Nkamia afunga mashindano Lukuvi Cup

 

Naibu Waziri aibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia akikabidhi zawadi ya kombe
Naibu Waziri aibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo,Juma Nkamia akikabidhi zawadi ya kombe

 

 

 

 

Hatimaye Mashindano ya Lukuvi Cup Kata ya Migori yamemalizika kwa timu ya Mtera Shooting kuibuka mabingwa wa kombe hilo kwa kuilaza timu ya Home Boys kwa jumla ya goli 4 kwa 1.

Akikabidhi zawadi kwa mshindi wa kwanza, wa pili na wa tatu, Naibu Waziri wa habari, vijana, utamaduni na michezo, Juma Nkamia,ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi, alisema kuwa vijana wengi Tanzania wanapenda michezo japo bado kuna tatizo kubwa kwa viongozi wa michezo hususani walimu wa timu kwa kutokuwa na mafunzo ya ualimu wa timu.

Nkamia alimkabidhi mshindi wa kwanza kombe na fedha taslimu shilingi 1,000,000, ambapo mshindi wa pili alikabidhiwa kombe na shilingi 500,000, huku mshindi wa tatu akiambulia shilingi 250,000.

Alisema kuwa lengo la mashindano hayo limetimia ambapo vijana wengi walihamasika kushiriki katika michezo tofauti na dhana potofu ya vijana kujihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya na ngono zembe.

28 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2014/11/19/naibu-waziri-nkamia-afunga-mashindano-lukuvi-cup/">
RSS