MKUTANO MKUU WA MWAKA WA KAMATI YA OLIMPIKI TANZANIA, TAREHE 13 Desemba,2014 MJINI MOROGORO.

MKUTANO MKUU WA MWAKA WA KAMATI YA OLIMPIKI TANZANIA,

TAREHE 13 Desemba, 2014 MJINI MOROGORO.

Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) inategemea kufanya Mkutano wake wa mwaka mjini Morogoro, tarehe 13 Desemba,2014 katika ukumbi wa Hoteli ya Kingsway.

Mkutano huu utahudhuriwa na Viongozi wa Vyama/Mashirikisho ya Michezo kutoka Tanzania Bara na Zanzibar ambao ni wanachama hai na halali wa kamati ya Olimpiki Tanzania, Wakurugenzi wa Michezo, Makatibu wa Mabaraza ya Michezo  Tanzania Bara na Zanzibar, Msajili kutoka Tanzania Bara na Mrajis kutoka Zanzibar.

Lengo la Mkutano ni kufanya tathmini ya shughuli na maendeleo ya michezo ambayo TOC imeifanya kwa mwaka  2014,  na unatarajiwa kuanza saa 2:30 asubuhi.

8 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2014/11/21/mkutano-mkuu-wa-mwaka-wa-kamati-ya-olimpiki-tanzania-tarehe-13-desemba2014-mjini-morogoro/">
RSS