MICHEZO YA JADI HAINA BUDI KUDUMISHWA

MICHEZO YA JADI HAINA BUDI KUDUMISHWA

Mshindi  wa mchezo wa bao mwaka 1988 Kitaifa mjini Shinyanga Athuman Seleman, akicheza na Bibi Zaitun Nasoro Lukinga matroni wa wanamchezo wa jadi ikiwa ni maandalizi ya Tamasha la Matema beach festiva

Mwenyekiti na Fundi wa michezo ya jadi,  Mohamed Kazingumbe  alisema wao kila siku wapo kwenye viwanja vyao kuendelea na mazoezi  ili kuleta ufanisi na kuiendeleza michezo ya jadi. Aliyasema haya akiwa katika mazoezi na wana michezo wa jadi pembeni ya uwanja wa Taifa zilipokuwa ofisi za Baraza la michezo la Taifa (BMT).

Aliendelea , sasa hivi tupo kwenye mazoezi  tukiwa kwenye maandalizi ya Tamasha la Matema beach Festival litakalofanyika Mbeya  kuanzia tarehe 27 Novemba,2014. Tamasha litakalohusisha michezo ikiwemo michezo ya Jadi, “alisema mzee kazingumbe”.

Alisema michezo tunayojihusisha nayo ni kucheza bao, kulenga shabaha, kusuka ukili, mdako, kukuna nazi  na mieleka. Michezo hii huhusisha rika tafauti.

Mwishoni mwa mwezi wa kumi (10) nilipata mwaliko nchini Korea kama Rais wa michezo ya jadi Afrika, ambapo kulikuwa na mashindano  ya michezo ya jadi. Mashindano yaliyohusisha nchi zaidi ya thelethini, Tanzania hatukuweza kupeleka timu yetu kutokana na ufinyu wa bajeti ila niliweza kuiwakilisha nchi yetu, “ alisema kazingumbe”.

Mzee kazingumbe alimalizia kwa kusema, hatuna budi kuiendeleza na kuithamini michezo ya jadi kama ilivyo michezo mingine kwani hata yenyewe inachezwa kitaifa na  kimataifa.

 

 

8 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2014/11/25/1180/">
RSS