SERIKALI YAKABIDHIWA ULINGO WA NGUMI

Serikali yakabidhiwa ulingo wa ngumi

Serikali imekabidhiwa ulingo wa kisasa wa mchezo wa ngumi na kampuni ya simu ya Zantel wakati Chama cha karate Tanzania kimefaidika kwa kupewa sh. Milioni 10 na kampuni hiyo.

Ulingo wa kimataifa uliotolewa kwa Serikali na Kampuni ya simu Zantel ili usaidie mchezo wa ngumi nchini
Ulingo wa kimataifa uliotolewa kwa Serikali na Kampuni ya simu Zantel ili usaidie mchezo wa ngumi nchini

Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bw. Henry Lihaya akitoa neno kwa watendaji wa Zantel kabla ya kumkaribisha Waziri
Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bw. Henry Lihaya akitoa neno kwa watendaji wa Zantel kabla ya kumkaribisha Waziri

Akieleza katika makabidhiano ya ulingo huo jana katika uwanja wa ndani wa Taifa,Waziri wa Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo, Dr. Fenella Mkangara alisema Kampuni ya Zantel wamesikia kilio chake cha kuinua sekta ya michezo.

Alifafanua kuwa baada ya kufikisha ombi lao kampuni hiyo iliwaeleza kuwa wataanza kuwasaidia katika michezo mitatu ambayo ni Ngumi, Wavu na Karate.

Dr. Fenella alisema, changamoto inayoikabili sekta ya michezo ni miundombinu hasa kwa upande wa ngumi ulingo wa kimataifa utakaosaidia katika mashindano mbalimbali ya kimataifa.

Alisema, alipata aibu baada ya kuhudhuria pambano la bondia Fransis  Cheka alipopigana na Mmarekani Phil Williams, ambapo aliulizwa maswali mengi na wageni walioongazana na bondia huyo kuhusu ulingo.

Waziri wa Habari, Vijana ,Utamaduni na Michezo Dr. Fenella Mkangara akiwa ulingoni baada ya kukabidhiwa na Mtendaji Mk uu wa Zantel Bw. Pratap Ghose
Waziri wa Habari, Vijana ,Utamaduni na Michezo Dr. Fenella Mkangara akiwa ulingoni baada ya kukabidhiwa na Mtendaji Mk uu wa Zantel Bw. Pratap Ghose

Alifafanua kuwa ulingo tuliopata utatumiwa na Shirikisho la Ngumi za ridhaa la Taifa (BFT)  pamoja na vyama vya ngumi vya mikoa kwa utaratibu utaowekwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT).

Cheki ya Shilingi Milioni kumi iliyokabidhiwa kwa Serikali na Kampuni ya simu ya Zantel kukisaidia Chama cha Kareti nchini.
Cheki ya Shilingi Milioni kumi iliyokabidhiwa kwa Serikali na Kampuni ya simu ya Zantel kukisaidia Chama cha Kareti nchini.

NGUMPIGANA

WASHABIKI

138 total views, 2 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by EmailO
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2014/12/11/serikali-yakabidhiwa-ulingo-wa-ngumi/">
RSS