MABARAZA MAPYA YA MICHEZO YAANZA KWA KASI MPYA NA ARI MPYA

MABARAZA MAPYA  YA MICHEZO YAANZA KWA KASI MPYA NA ARI MPYA

Wenyeviti wa Mabaraza ya Michezo Tanzania Bw. Dioniz Malinzi wa (BMT) na Bibi Sharifa Hamisi wa (BMZ) wameanza kwa Kasi Mpya na Ari Mpya, baada ya Uzinduzi  kuanza na kikao kazi cha pamoja kwa Mabaraza yote Mjini Zanzibar mwishoni mwa mwezi.

Mwenyekiti wa Baraza la michezo Tanzania Bw. Dioniz Malinzi (shati jeupe) na baadhi ya wajumbe wakielekea kwenye kikao cha pamoja cha Mabaraza ya Michezo ya Tanzania Bara na Zanzibar
Mwenyekiti wa Baraza la michezo Tanzania Bw. Dioniz Malinzi (shati jeupe) na baadhi ya wajumbe wakielekea kwenye kikao cha pamoja cha Mabaraza ya Michezo ya Tanzania Bara na Zanzibar

Akizungumza katika kikao hicho,  Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bw.  Dioniz Malinzi alisema, Mabaraza yote lazima tufanye kazi kwa pamoja  na kuwa na mikakati ya kumaliza migogoro baina ya Timu zetu za Taifa, Vyama na Vilabu   kwa maendeleo ya Michezo nchini ili tupata Medali katika mashindano ya Kitaifa na Kimataifa.

Mabaraza yote haya  lazima tuwe na ratiba ya Vikao vya pamoja ili kubadilishana mawazo, kushauriana na kuangalia njia sahihi ya wanamichezo wa Tanzania kutumia rasilimali zilizopo ili tuhakikishe tunaboresha maendeleo ya michezo nchini, kama  bahari na maziwa kwa waogoleaji lazima watengewe maeneo ya mazoezi, “ alisema malinzi.”

Wajumbe wa Mabaraza  yote mawili BMT na BMZ  walikubaliana kuwa lazima wawe wanajitathmini kwenye vikao vyao kuona mafanikio na changamoto zilizokwamisha maendeleo ya michezo nchini.

Kikao kilihudhuriwa na wenyeviti wa Mabaraza ya michezo, Makatibu wakuu na wajumbe wa kutoka (BMT) na (BMZ).

vlcsnap-2015-02-06-09h45m44s60

Wenyeviti na Wajumbe wa Mabaraza ya michezo ya  Tanzania Bara na  Zanzibar  wakiwa  kwenye kikao cha pamoja wakijadili jinsi ya kuiendeleza michezo nchini na hatimaye kupata medali katika mashindano ya Kitaifa na  Kimataifa, kikao kilichofanyika Zanzibar mwishoni mwa mwezi wa kwanza.

Wenyeviti wa Mabaraza ya Michezo Tanzania bara na Zanzibar Bw. Dioniz  Malinzi wa Bara na Bibi Sharifa Hamisi wa Zanzibar na Mjumbe wa (BMT) Mohamed Bawazir wakijadili jambo baada ya kutoka katika kikao kazi  kilichofanyika Zanzibar mwishoni mwa mwezi.

7 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2015/02/06/mabaraza-mapya-ya-michezo-yaanza-kwa-kasi-mpya-na-ari-mpya/">
RSS