TANZANIA MWENYEJI WA MASHINDANO YA KOMBE LA AFRIKA NETBOLI

DSC03328

 

 

 

 

 

 

 

TANZANIA MWENYEJI WA MASHINDANO YA KOMBE LA AFRIKA NETBOLI

Chama cha Netiboli Tanzania (CHANETA) kimekubali kuwa mwenyeji wa mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika yatakayofanyika kuanzia Machi 16, mwaka huu.

Tanzania imepata fursa hiyo baada ya Zambia kushindwa kupokea uwenyeji huo kama ilivyokuwa imepangwa awali. Michuano hiyo inaweza kufafanishwa na michuano maarufu iliyohitimishwa mwanzoni mwa mwezi huu nchini Equatorial Guinea ijulikanayo kama AFCON.

Akielezea, Mwenyekiti wa CHANETA Mama Anne Kibira, alisema kuwa walipokea ombi la kuwa mwenyeji wa Kombe hilo mwanzoni mwa mwezi na hawakusita wamelikubali.

Alifafanua kuwa Chama cha Netiboli Afrika (AN) kimepanga kushirikiana na uongozi wa shirikisho la Mchezo huo duniani (INF) kuipa ushirikiano Tanzania kutimiza kiu yao kuwa mwenyeji wa michuano hiyo mwaka huu.

Aliendelea kwamba Tanzania kuteuliwa kuandaa mashindano hayo,  ni kutokana na imani waliyo nayo  viongozi wa mchezo huo Kimataifa kwa  Chama cha Netiboli Tanzania (CHANETA).

Mwenyekiti wa CHANETA Mama Kibira, “alisema, hadi sasa hatujathibitishiwa ni nchi ngapi zitashiriki katika Kombe hilo, ambalo litahusisha timu mbalimbali za Bara la Afrika.

Nafasi tuliyopata ni kubwa na muda wa maandalizi ni mdogo, tunaomba wadau  kutupa ushirikiano ili kufanikisha michuano hiyo, “alisema Mama Kibira.

Timu ya Taifa ya Netiboli  “Taifa Queens”  ipo katika nafasi ya nne katika viwango vya ubora wa Timu za Netiboli za Afrika na nafasi ya 15 katika viwango vya Timu za dunia kulingana na takwimu za mwishoni mwa mwaka jana. Tunawaahidi wadau kufanya maandalizi ya kutosha ili timu yetu ifanye vizuri katika mashindano hayo, “alisema Mama Kibira.”

67 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2015/02/11/tanzania-mwenyeji-wa-mashindano-ya-kombe-la-afrika-netboli/">
RSS