TANZANIA YASAINI MAKUBALIANO YA IWG

Tanzania yaridhia waraka wa makubaliano wa Brighton Declaration katika kuleta msukumo wa ushiriki wa wanawake na usawa wa kijinsia katika michezo.

Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo, Bibi Juliana Yassoda akieleza jambo kuhusu Makubaliano ya ‘ Brighton Declaration’ kabla ya kusainiwa kwa Makubaliano hayo.
Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo, Bibi Juliana Yassoda akieleza jambo kuhusu Makubaliano ya ‘ Brighton Declaration’ kabla ya kusainiwa kwa Makubaliano hayo.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Maridhiano hayo yamefikiwa jana jijini Dar es Salaam ambapo  Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Henry Lihaya alitia saini Waraka huo huku akishuhudiwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo Bibi. Juliana Yassoda

Katibu Mkuu (BMT) Bw. Henry Lihaya akisaini Makubaliano ya “ Brighton Declaration” ya usawa wa kijinsia katika Michezo.
Katibu Mkuu (BMT) Bw. Henry Lihaya akisaini Makubaliano ya “ Brighton Declaration” ya usawa wa kijinsia katika Michezo.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Akizungumza mara baada ya kutia saini waraka huo Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Henry Lihaya alisema kuwa imekuwa faraja  Serikali kuridhia waraka huo kwa kuwa utaongeza fursa kwa wanawake wengi zaidi kushiriki katika michezo mbalimbali ndani na nje ya nchi.

“Akizungumza baada ya kusaini Makubaliano hayo Bw. Lihaya, “ alisema hii itakuwa fursa kubwa kwa nchi yetu kuwashirikisha Wanawake na Wasichana katika Michezo Kimataifa, kwani watashiriki kiurahisi zaidi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Juliana Yassoda amesema kuwa ni wakati muafaka sasa kwa Tanzania kutoa fursa  kwa wanawake kushiriki kikamilifu katika masuala mbalimbali yanayohusu michezo, hivyo kuridhia Waraka huu ni jambo jema kwa maslahi ya michezo nchini.

Katibu Mkuu (BMT) Bw. Henry Lihaya akielezea umuhimu wa michezo kwa wanawake baada ya kusaini makubaliano ya “Brighton Declaration”
Katibu Mkuu (BMT) Bw. Henry Lihaya akielezea umuhimu wa michezo kwa wanawake baada ya kusaini makubaliano ya “Brighton Declaration”

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Yassoda aliongeza kuwa kutokana na Tanzania kuridhia waraka huo sasa wanamichezo wanawake watapata fursa zaidi za kushiriki katika michezo ikiwemo kuhudhuria makongamano ya wanamichezo wanawake yanayoratibiwa na Chama cha Kimataifa cha Wanawake na Michezo (IWG) ambapo kila baada ya miaka minne hukutana na kujadiliana masuala mbalimbali kuhusu  michezo na wanawake.

Aidha Yassoda alibainisha kuwa makubaliano hayo yalifikiwa tokea mwaka 1994 ambapo nchi mbalimbali duniani kote zimekuwa zikitekeleza makubaliano hayo, ikiwemo Tanzania na kuongeza kuwa Serikali imeona ni muda muafaka sasa wa kuridhia rasmi waraka huo ili kuleta hamasa ya wanawake katika michezo.

Waraka wa Brighton Declaration ni makubaliano ambayo yamelenga kutoa msukumo kwa Serikali, Taasisi za kirai na mashirikia ya kijamii kutoa kipaumbele kwa wanawake kushiriki katika shughuli mbalimbali zinazohusu michezo ili kuleta usawa wa kijinsia katika sekta hiyo. Tanzania imeridhia rasmi makubaliano hayo  tarehe 12 Februari, 2015.

 

 

 

 

43 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2015/02/13/tanzania-yasaini-makubaliano-ya-iwg/">
RSS