TANZANIA IMETESA MASHINDANO YA JUDO A. MASHARIKI 2015

TANZANIA IMETESA  MASHINDANO YA JUDO A. MASHARIKI

Katibu Mkuu Chama cha Mchezo wa Judo, Innocent Malya, “ alipotembelea Ofisi za (BMT) alisema kikosi chake cha Tanzania Bara  kimetwaa ubingwa katika mashindano ya Timu za Afrika Mashariki yaliyomalizika mwishoni mwa wiki Chuo cha Mafunzo ya Polisi  (CCP) Mkoani Kilimanjaro.

 

IMG-20150219-WA0010 - Copy

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Malya alisema, shindano hilo lilishirikisha  timu kutoka Zanzibar, Kenya, Burundi , Rwanda na Ethiopia, ambapo Tanzania Bara imetetea ubingwa huu kwa mara ya tatu mfululizo na kujinyakulia medali nne za dhahabu, moja ya fedha na nne za shaba wakati mshindi wa pili amechukua Zanzibar ambao wamechukua medali mbili za dhahabu, nne za fedha na tatu za shaba.

Aliendelea kuwa, nafasi ya tatu ilichukuliwa na Burundi  waliobeba medali moja ya dhahabu, nne fedha na tatu za shaba wakati Kenya ikishika mkia katika mashindano hayo na kuambulia fedha tano na shaba saba.

IMG-20150219-WA0008

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Mashindano hayo yalidhaminiwa na Mfuko wa Akiba wa (GEPF), tunomba Serikali, Mashirika na Wadau kujitokeza kudhamini mashindano ili kutoa hamasa kwa wachezaji na kwa maendeleo ya mchezo wa Judo Tanzania,” alisema Malya.”

IMG-20150219-WA0007

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Katibu Mkuu wa Judo, “ alisema tuna mashindano kapambe yako mbele yetu mwezi June nchini Burundi ya umri wa miaka chini ya 21 yajulikanayo kama ‘Junior’ na chini ya miaka 17 yaitwayo‘ Cardet.’ Ambapo mwezi Septemba tutakuwa na shindano la “All African game” nchini Congo Brazaville,  tunaomba Serikali,  Wadhamini  na  Wadau kutupa nguvu ya kutimiza ndoto zetu, “alisisitiza Innocent.”

20 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2015/02/19/tanzania-imetesa-mashindano-ya-judo-a-mashariki/">
RSS