CHAMIJATA YAHAHA NA MDHAMINI WA SAFARI YA CHINA

CHAMIJATA YAHAHA NA MDHAMINI WA SAFARI YA CHINA

Chama cha Michezo ya Jadi Tanzania “CHAMIJATA” kinahaha  kupata mdhamini wa wakukiwezesha kushiriki tamasha la kimataifa la Mchezo wa Jadi lijulikanalo kama “World Traditional Archele Festival” linalotarajiwa kufanyika machi mwaka huu nchini China.

CHAMIJAPIC

 

 

 

 

 

 

 

Akizungumza kwa simu, Mwenyekiti wa Chama cha michezo ya Jadi, Mohamed Kazingumbe, “alisema, tumetuma maombi kwa watu zaidi ya 15 ili kupata mdhamini wa safari hiyo, ila bado  hatujapata mrejesho ili kujihakikishia ushiriki wetu katika Tamasha hilo.

Alieleza kuwa leo/jana jioni watakuwa na kikao na viongozi wa Chama ili kujua maendeleo ya mchakato wa kumpata mdhamini wa kufanikisha safari hiyo.

BAO

 

 

 

 

 

 

 

Mzee Kazingumbe alisema kuwa wanatarajia kusafirisha wachezaji wanane (8) na viongozi wanne (4) ambapo safari inagharimu milioni 40, vilevile Septemba mwaka huu pia tumealikwa nchini Korea kwenye shindano la michezo ya jadi, ombi letu kwa Serikali na wadhamini ni kutupa ushirikiano ili kufanikisha safari za michezo kwa maendeleo ya michezo na nchi kujitangaza.

45 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2015/02/26/chamijata-yahaha-na-mdhamini-wa-safari-ya-china/">
RSS