TANZANIA KUMINYANA NA MISRI UFUKWENI IJUMAA

TANZANIA KUMINYANA NA MISRI UFUKWENI IJUMAA

Timu ya Taifa ya Tanzania ya soka la ufukweni (Beach Soccer) inatarajiwa kucheza na timu ya Taifa ya Misri siku ya ijumaa majira ya saa 10 kamili jioni, mchezo utakofanyika katika klabu ya Escape 1 Msasani jijini Dar es salaam.

Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania kinaendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo huo, ambapo kwa takribani wiki mbili kipo kambini Bamba Beach wakijifua kwa mchezo huo.

Timu ya Taifa ya Soka la ufukweni ya Tanzania
Timu ya Taifa ya Soka la ufukweni ya Tanzania

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Tanzania ilifuzu hatua ya pili baada ya kuichapa timu ya Taifa ya Kenya kwa jumla ya mabao 12 kwa 9,  na endapo itafanikiwa kuwaota Misri, itafuzu moja kwa moja kucheza Fainali za soka la Ufukweni zitakazofanyika Visiwa vya Shelisheli mwezi April mwaka huu.

 

36 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2015/03/12/tanzania-kuminyana-na-misri-ufukweni-ijumaa/">
RSS