YANGA YAICHARAZA FC PLATINUM

YANGA YAICHARAZA FC PLATINUM

 Kikosi cha Yanga
Kikosi cha Yanga

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Dar es salaam, Yanga imepiga hatua mbele baada ya kuicharaza FC Platinum ya Zimbabwe kwa bao 5-1 na kujiweka katika mazingira mazuri ya kusonga mbele kwa hatua ya pili ya mashindano ya Kombe la Shirikisho la Afrika.

Ikitimua vumbi mbele ya mashabiki wake kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam jana,  Yanga iliwakonga moyo mashabiki kwa kile walichosubiri kwa hamu kubwa ambapo iliichapa Timu ya Zimbabwe kwa mabao matano kwa moja na kusafisha njia yake kusonga mbele.

Mabao ya Yanga yalifungwa na Salum Telela, Haruna Niyonzima, Amisi Tambwe na Mrisho Ngassa aliyefunga mabao mawili, huku Walter Musoma akifunga bao la kufuta machozi kwa Platinum.

Endapo Yanga itashinda mchezo wa marudiano utakaotimua vumbi wiki mbili zijazo jijini Bulawayo- Zimbabwe itafanikiwa kucheza na mshindi kati ya Benfica de Luanda ya Angola na Etoile Sahel ya Tunisia, hali ya kuwa Watunisia wakipewa nafasi kubwa baada ya kushinda mechi ya kwanza bao 1-0.

Yanga ilianza mechi jana kwa kasi ikiwatumia washambuliaji wake wenye kasi Ngassa na Msuva kushambulia lango la Platinum waliokuwa wakicheza kwa umakini mkubwa.

Tambwe alikosa bao dakika ya 17, kwa kuchelewa kuunganisha krosi ya Msuva, kabla ya Niyonzima kupiga shuti ndakika ya 22 na kutoka pembeni kidogo ya lango la Platinum baada ya kuokolewa na beki Kelvin Moyo.

Dakika ya 31, kiongo Telela aliwainua mashabiki wa Yanga baada ya kupokea pasi kutoka kwa Mbuyu Twite na kuunganisha shuti la umbali wa mita 35, lililoenda moja kwa moja wavuni  na kumwacha kipa wa Platinum, Patros Mhari mdomo wazi.

Yanga ikiendelea kuwatesa Platinum ilijipatia bao la pili dakika ya 41 lililopachikwa na Niyonzima akimalizia mpira uliotemwa na kipa Mhari aliyepangua shuti la Tambwe.

Baada ya bao hilo Platinum walijiweka sawa na kuanza kucheza soka la kushambulia ambapo walipata bao dakika ya 45, bao lililofungwa na Musoma kwa mpira wa adhabu nje kidogo ya eneo la 18, iliyokwenda moja kwa moja wavuni na kumwacha Mstapha ‘Barthez’ kipa wa Yanga asijue la kufanya.

Kikosi cha FC Platinum ya Zimbabwe
Kikosi cha FC Platinum ya Zimbabwe

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Yanga ilirudi kwa nguvu mpya kipindi cha pili na dakika ya 46, Tambwe alipachika bao la tatu akimalizia pasi ndefu iliyopigwa na Ngassa na kuwazidi mbio mabeki nwa Platinum na kupiga shuti lililoingia wavuni.

Wanajangwani waliendelea kutawala mchezo na kupata bao la nne dakika ya 52 lilipachikwa na Ngassa baada kupokea pasi kutoka kwa Juma Abdul na Tambwe aliyepitisha pasi ya mwisho kwa mfungaji.

mrisho

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Kocha wa Yanga, Hans Pluijm aliwapumzisha Msuva, Juma Abdul na kuwaingiza Kpah Sherman na Hassan Dilunga katika kuihakikishia timu yake maendeleo mazuri. Dakika ya 88, Dilunga alipiga shuti lililopanguliwa na kipa na kuwa kona ambayo iliokolewa na mabeki wa Platinum, lakini Sherman aliuwahi mpira huo na kutoa pasi kwa Ngassa ambaye hakufanya makosa na kupachika goli la tano na kuwafanya Wazimbabwe kuishiwa nguvu.

Mashabiki wa yanga
Mashabiki wa yanga

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Baada ya mechi kumalizika, kocha Pluijm aliwasifu wachezaji wake kwa kucheza vizuri kwa kufuata maelekezo.

“Kasi ya Ngassa, Msuva  na Tambwe imesaidia kufanya mchezo kuwa mwepesi na kupata ushindi huu.”

18 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2015/03/16/yanga-yaicharaza-fc-platinum/">
RSS