TANZANIA YAFUNGWA 6-2 NA MISRI SOKA LA UFUKWENI

TANZANIA YAFUNGWA 6-2 NA MISRI SOKA LA UFUKWENI

Timu ya Taifa ya Tanzania Soka la Ufukweni imeanza vibaya katika michuano ya kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika, baada ya Misri kuibuka na mabao 6-2 katika ufukwe wa Escape One, Mikocheni, Dar es salaam.

tanzaniaed

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Matokeo hayo yataipa mzigo timu ya Tanzania katika mechi ya marudiano wiki ijayo nchini Misri, ambapo watatakiwa kushinda kwa wastani wa mabao matano zaidi ugenini.

Katika mechi hiyo, Tanzania ilianza vizuri na kuongoza robo ya kwanza kwa mabao 2-1,  kabla ya kibao kuwageukia robo ya pili na kutoka mapumziko wakiwa nyuma kwa mabao 3-2.

editedmisri
Mchezaji wa timu ya taifa ya Misri ya soka la ufukweni, Ibrahim Mohammed (kushoto) akimtoka mchezaji wa Tanzania katika mechi ya kwanza Raundi ya Pili kufuzu Fainali za Afrika jana ufukwe wa Escape One, Mikocheni, Dar es Salaam. Misri ilishinda 6-2.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Katika robo ya tatu jahazi la Tanzania linalopata mafunzo yake kutoka kwa beki wa zamani wa kimataifa nchini, John Jacob Mwansasu aliyewika Yanga SC, lilizidi kuzama baada ya kumaliza ikiwa nyuma kwa mabao 4-2.
Robo ya mwisho iliwamaliza kabisa Tanzania baada ya timu ya Misri kuongeza mabao mengine mawili, hivyo kulala na 6-2.
Mabao ya Tanzania yalifungwa na Ally Rabbi na Mwalimu Akida, wakati mabao ya Misri yalifungwa na Islam Ahmed, Yahia Ally manne na Mohammed Faway.
tanzania2ed
 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Huu ni mwaka wa kwanza, Tanzania inashiriki michuano ya soka la ufukweni na haina Ligi ya maana tayari ya kuzalisha wachezaji, Hivyo Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) linahitaji kuwekeza zaidi katika mchezo huu ili kujihakikishia matokeo mazuri katika mashindano yoyote.

Katika Raundi ya kwanza, Tanzania iliitoa Kenya kwa kuifunga nyumbani na ugeni

19 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2015/03/17/tanzania-yafungwa-6-2-na-misri-soka-la-ufukweni/">
RSS