MGOGORO TTA WAPATIWA SULUHISHO

MGOGORO TTA WAPATIWA SULUHISHO

Kamati ya Nidhamu, Usuluhishi na Rufaa ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT)  kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Leonard Thadeo wamekaa kikao na Kamati ya Utendaji ya Chama cha Mpira wa Tenisi (TTA)kupata suluhu ya mgogoro ulioripotiwa na wanachama kuhusu Uongozi wa chama hicho, kikao kilichofanyika machi 24, 2015  katika Ukumbi wa BMT.

Bw. Thadeo akiwa kwenye picha ya pamoja na  Kamati ya Nidhamu,Usuluhishi na Rufaa (BMT) na Viongozi wa TTA baada ya kumalizika kwa kikao.
Bw. Thadeo akiwa kwenye picha ya pamoja na Kamati ya Nidhamu,Usuluhishi na Rufaa (BMT) na Viongozi wa TTA baada ya kumalizika kwa kikao.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Aliendelea kuwa, kwa mujibu wa maelezo ya Katibu wa Baraza la Michezo Bw. Henry Lihaya, Uongozi wa chama cha Tenisi uliandikiwa zaidi ya barua tatu (3)  kuhusu tuhuma hizo na BMT lakini hawakujibu barua hizo.  Katibu  aliamua kumweleza Mwenyekiti wa Baraza Bw. Dioniz Malinzi juu ya suala hilo, ambapo aliagiza  wafahamishwe  kutaka kufanya kikao nao  pia hawakufika na hawakutoa taarifa yoyote.

Kamati ya Utendaji ya Chama cha Tenisi (TTA) imekiri uwepo kwa migogoro na kukubali makosa waliyofanya kwa BMT, ambapo kwa niaba ya Uongozi  wa Chama cha Tenisi, Katibu Mkuu  Bw.William Kallaghe aliiomba radhi mamlaka ya BMT ambapo,  Katibu wa Baraza la Michezo la Taifa Bwana Lihaya  alipokea msamaha huo bali aliomba uletwe kwa maandishi.

Kamati ya Nidhamu, Usuluhishi na Rufaa ilifikia maamuzi kuwa chanzo cha migogoro yote ni Ulegevu wa katiba iliyopo na kutokuwepo kwa Rais, kufuatia Rais aliyekuwepo Bw. Mbajo kujiuzulu.

TTA waliagizwa mambo haya yatekelezwe, Kamati ya Utendaji kufanya mkutano wa ndani na baadaye wafanye mkutano na vyama na vilabu na wadau wa  Tenisi na waeleze maazimio ya kikao hiki, waitishe uchaguzi mdogo ili kumpata Rais, na  wakutane na Uongozi wa Baraza la Michezo (BMT) kufanya maboresho ya Katiba na kuiwasilisha kwa Msajili ili iwe tayari kwa matumizi.

Ambapo, Katibu wa Baraza la Michezo la Taifa Bw. Henry Lihaya, alisema kuwa maazimio ya kikao yataandaliwa na kila mjumbe atatumiwa, ambayo yatawaongoza Viongozi wa Chama cha Tenisi (TTA) katika utekelezaji wa maazimio hayo.

Kabla ya kuhitimisha kikao hicho, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Bw.Thadeo aliwashauri viongozi wa Chama cha Tenisi kuaminiana na kuainisha wanachama wa msingi wa Tenisi na wenye mapenzi ya dhati na mchezo huo ili kujihakikishia maendeleo ya mchezo wa Tenisi katika nchi yetu.

Kikao cha usuluhishi kilihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Barara la Michezo la Taifa (BMT) Bw. Lihaya, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Bw. Leonard Thadeo, Mjumbe na Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu, Usuluhishi na Rufaa ya BMT Jamal Rwambo, Afisa michezo Halima Bushiri, Afisa Habari Najaha Kadri.

Wengine ni Makamu wa Rais Fina Mango, Katibu Mkuu William Kallaghe, Katibu Mkuu Msaidizi Joshua M.Mutale na  Mjumbe Hassan Kassim  kutoka Chama cha Tenisi Tanzania (TTA)

30 total views, 2 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2015/03/25/mgogoro-tta-wapatiwa-suluhisho/">
RSS