MTANZANIA AIBUKA KIDEDEA

MTANZANIA AIBUKA KIDEDEA

Bondia Mtanzania, Mohamed Matumla aliipa sifa Tanzania na Watanzania baada ya kumpa kichapo Mchina, Wang Xin Hua, katika pambano la Super Bantam lililofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee machi 27, 2015.

Bondia Mohamed Matumla amemchapa mpinzani wake raia wa China, Wang Xin Hua kwa pointi. Matumla ameshinda pambano hilo la kuwania ubingwa wa dunia wa WBF la raundi 12 uzani wa Bantam lililopigwa katika Ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.
Bondia Mohamed Matumla amemchapa mpinzani wake raia wa China, Wang Xin Hua kwa pointi. Matumla ameshinda pambano hilo la kuwania ubingwa wa dunia wa WBF la raundi 12 uzani wa Bantam lililopigwa katika Ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Bondia Mohamed Matumla amemchapa mpinzani wake raia wa China, Wang Xin Hua kwa pointi. Mtanzania huyo ameshinda pambano hilo la raundi 10 uzani wa Bantam lililopigwa katika Ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.

Kabla ya mpambano huo uliowavuta mashabiki wengi, Matumla aliwaeleza mashabiki kuwa amejiandaa vya kutosha na anawahakikishia ushindi Watanzania na uwanjani anaenda kuhitimisha tu ushindi, ukweli ambao ameuonyesha.

Katika mpambano huo uliochukua raundi 10, Matumla alionyesha uwezo mkubwa tangu raundi ya kwanza, ambapo majaji hawakupata shida kumpa pointi Mtanzania huyo dhidi ya mpinzani wake kutoka China.

Jambo la kufurahisha katika pambano hilo ni jinsi mashabiki walivyofurika katika Ukumbi huo na kumpa faraja  mpambanaji huyo.  Ambapo watazamaji  wamefurahishwa na ushindi huo kwani sio furaha kwa familia ya Matumla pekee bali furaha na faraja kwa nchi nzima kwani kaipa sifa Tanzania.

Kwa muda mrefu Tanzania tumeshindwa kuvuka hatua linapokuja suala la michezo ya kimataifa, hali ambayo imekuwa ikiwakatisha tamaa wadau wa michezo mbalimbali na sasa Matumla ameamsha ari ya wapenzi wa masumbwi.

18 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2015/03/29/jr-matumla-marekani-hiyoo/">
RSS