TANZANIA YANG’ARA RIADHA DUNIA

TANZANIA YANG’ARA RIADHA DUNIA

Tanzania imefanikia kung’ara katika mashindano ya riadha ya dunia yaliyofanyika mwishoni mwa wiki nchini China, baada ya kufanikiwa kushika nafasi ya sita kidunia.

RIADHA TANZANIA

Timu ya Tanzania iliongozwa na mwanariadha Ismail Juma aliyeshika nafasi ya tisa baada ya kukimbia kwa dakika 33.55 akifuatiwa na Fabiano Nelson Sulle aliyeshika nafasi ya 33 aliyekimbia kwa dakika 37.26.

Huku mkimbiza upepo Joseph Panga akiibuka nafasi ya 40 baada ya kutumia dakika 37.43, akifuatiwa  na Alphonce Felix aliyeibuka katika nafasi ya 48 akitumia dakika 38.07  na wa mwisho  kwa upande wa Tanzania akiwa ni John Bazil aliyeshika nafasi ya 65 akikimbia kwa dakika 38.44.

Matokeo haya yameifanya Tanzania kuibuka kidedea katika nafasi ya sita duniani  wakati ubingwa wa jumla ukichukuliwa na Ethiopia, ikifuatiwa na Kenya, Bahrain, Eritrea na Uganda.

Baada ya ushindi huo, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Suleiman Nyambui,  “alisema  ushindi huo ulitokana na wanariadha hao kufanya mazoezi kwa pamoja kwa muda mrefu chini ya kocha mmoja.

“Wanariadha hao watakaporejea nchini Kamati ya ufundi ya RT itakutana na klabu zao ili kupanga jinsi gani watakavyolinda viwango vya wakimbiaji wetu visishuke,” alisema Nyambui.

 

93 total views, 2 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2015/03/30/tanzania-yangara-riadha-dunia/">
RSS