TAARIFA ZA KIMICHEZO KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TFF

TAARIFA ZA KIMICHEZO KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TFF

TFFlogo

Timu ya Taifa ya Tanzania ya Vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U-15) imeingia kambini leo katika hoteli ya Itumbi iliyopo magomeni chini ya kocha mkuu Adolf Rishard kujiandaa na progamu ya vijana kuwania kufuzu kwa fainali za U-17 mwaka 2017 nchini Madagascar.

Akiongea na waandishi wa habari jana kwenye ukumbi wa habari wa TFF Karume, mwenyekiti wa kamati ya soka la vijana Bw. Ayoub Nyenzi amesema kamati yake imeandaa programu maalumu ya kuwaanda vijana kwa ajili ya kuichezea timu ya Taifa U-17 mwaka 2017.

TFF imeandaa program hiyo ya vijana U-15 ambao watakua kambini kwa muda siku 10, wakifanya mazoezi uwanja wa Karume na kucheza michezo kadhaa ya kirafiki na timu za Azam U17 na shule ya Sekondari Makongo.

Kocha mkuu na timu yake ya U-15 atazunguka mikoa saba nchini kwa ajili ya kucheza michezo kadhaa ya kirafiki na kuibua vipaji vitakavyosaidia kuboresha timu yake. Mikoa itayotembelewa ni Mbeya, Mwanza, Morogoro, Arusha, Tanga, na Dar es alaam (Ilala, Kinondoni, Temeke).

Aidha katika kuhakikisha timu hiyo inakua tayari kwa michuano ya kuwania kufuzu kwa fainali za U-17 mwaka 2017 nchini Madagascar, timu hiyo ya vijana itafanya ziara ya mafunzo mwezi Disemba mwaka huu katika nchi za Malawi, Zambia, Zimbambwe, Botswana na Afrika Kusini kwa kucheza michezo ya kirafiki.

Mwezi Februari 2016 timu hiyo itacheza michezo miwili ya kirafiki na timu za mikoa ya Dodoma na Mwanza, kabla ya kuelekea  katika  ziara kwenye nchi za Burundi, Rwanda, Uganda na Kenya mwezi Aprili 2016.

Ratiba ya CAF kuwania kufuzu kwa fainalizaAfrika 2017 inatarajiwa kuanza mwezi Juni 2016, ambapo kikosi cha Tanzania kitakuwa kimeshapata muda mzuri wa maandalizi kwa lengo la kuhakikisha timu inashiriki fainali hizo nchini Madagascar 2017.

Fainali za U-17 mwaka 2017 zinatarajiwa kufanyika nchini Madagascar, huku Tanzania ikitarajia  kuwa mwenyeji wa fainali hizo za vijana U-17 mnamo mwaka 2019.

Jumla ya wachezaji 30 wameitwa kuingia kambini, wachezaji hao ni Kelvin Deogratius, Magazi Dotto, Anthon Shilole (Geita), Sadik Sud Ramadhani , Mwinchumu Yahya(Tanga),Faraji John, David Mbakazi , Juma Juma, Pius Raphael, Davison Meddy, Maulid Lembe (Dodoma), Ibrahim Koba (Morogoro).

Wengine ni Abubakar Badru Nassoro, Yusuf B.A. Khalfani, All Hafidh Mohamed (Kusini Pemba), Joachim Mwenda, Charles Cassiano, Luqman Shauri (Tanga), Juma Zuberi (Kigoma), Ismail Abdallah (Kusini Pemba), Robert Philipo (Arusha), Alex Peter, Mohamed Ally, Rashid Kilongola (Kinondoni), Saad Juma (Mkoa Magharibi), Ibrahim Shamba (Kusini Unguja), Ally Msengi, Klevin S.Kijili (Mwanza), Frank Abel (Simiyu) na Bryan Jamal.

 

53 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2015/04/08/taarifa-za-kimichezo-kutoka-shirikisho-la-mpira-wa-miguu-tff/">
RSS