TAIFA STARS KWENDA AFRIKA KUSINI LEO

TFFlogo

TAIFA STARS KWENDA AFRIKA KUSINI LEO

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) leo jumatano inatarajiwa kusafiri kuelekea nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kushiriki michuano ya kombe la COSAFA.

150510202601_kocha_wa_taifa_stars_nooij_512x288_bbc_nocredit

Michuano ya COSAFA inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Mei 17 mpaka Mei 30, 2015 katika viwanja vya Olympia Park na Moruleng jimbo la North West Province nchini Afrika Kusini ikishirikisha nchi za Kusini mwa Afrika huku Tanzania na Ghana zikiwa ni nchi waalikwa.

Taifa Stars inaondoka jijini Dar es salaam leo majira ya saa 1 jioni, kwa usafiri wa shirika la ndege la Fasjet ambapo wanatarajia kuwasili  jijini Johanesburg saa 5 usiku.

Mara baada ya kupimwa afya juzi na madaktari wachezaji Aishi Manula, Isihaka Hassan, Haroun Chanongo, Kelvin Friday na nahodha Nadir Haroub wamekutwa na majeruhi ambayo yamepelekea kutokuwepo katika kikosi kitakachosafiri leo, watabakia nchini wakiendelea kufanya mazoezi chini ya uangalizi mpaka timu itakaporejea kutoka Afrika Kusini na kuungana kwa ajili ya maandalizi ya AFCON, huku Amri kiemba akipewa ruhusa kutokana na kuwa na matatizo ya kifamilia.

Msafara wa Taifa Stars utaongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa TFF, Ephaphra Swai ukijumuisha wachezaji 20 na benchi la ufundi, timu inatarajiwa kufikia katika hoteli ya Sun City iliyopo pembeni kidogo ya jiji la Rusterburg.

Kesho siku ya Alhamis kuanzia saa 3 asubuhi mpaka saa 7 mchana wachezaji watakuwa mapumziko.


20 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2015/05/13/taifa-stars-kwenda-afrika-kusini-leo/">
RSS