CECAFA WATOA RATIBA KAGAME 2015

CECAFA WATOA RATIBA KAGAME  2015

Rais wa CECAFA Leodegar Tenga (katikati), Katibu Mkuu wa CECAFA Nicholas Musonye  (kushoto) na Rais wa  rais TFF Jamal Malinzi wakiwa katika Mkutano na vyombo vya Habari mwanzoni mwa wiki.
Rais wa CECAFA Leodegar Tenga (katikati), Katibu Mkuu wa CECAFA Nicholas Musonye (kushoto) na Rais wa rais TFF Jamal Malinzi wakiwa katika Mkutano na vyombo vya Habari mwanzoni mwa wiki.

Rais wa Baraza la Vyama vya Soka kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati, Leodgar Tenga jana ametangaza kuanza kwa michuano ya kombe la Kagame itakayoanza kutimua vumbi Julai 18, 2015 na kumalizika Agosti 2 mwaka huu jijii Dar es salaam. Pamoja  na kutangaza kuanza kwa michuano hiyo, Tenga ameishukuru serikali ya Tanzania na TFF kwa kukubali kuwa wenyeji wa michuano hiyo mikubwa, vyombo vya habari na wapenzi wa mpira wa miguu nchini kwa sapoti yao na kuipokea kwa mikono miwili michuano hiyo.

Tenga ameongeza kuwa lengo la CECAFA ni kuona vilabu vya ukanda huu vinapata nafasi ya kucheza michezo mingi na kujiandaa kwa ajili ya michuano ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho barani Afrika.

Katika hatua nyingine Rais wa TFF, Jamal Malinzi amewashukuru CECAFA kwa kuipa Tanzania uenyeji huo na kuahidi TFF kuwa  itahakikisha michuano hiyo inafanyika nchini katika hali ya amani na usalama toka mwanzo hadi kuhitimishwa kwa michuano hiyo.

Timu zilizothibitisha kushiriki michuano hiyo ni Yanga, Azam (Tanzania), APR (Rwanda), Gor Mahia (Kenya), Telecom (Djibout), KMKM (Zanzibar), Khartoum-N (Sudan), Al Shandy (Sudan) LLB AFC (Burundi), Heegan FC (Somalia), Malakia (Sudani Kusini), Adama City (Ethipia) na KCCA (Uganda).

Wakati huo Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholaus Musonye ametangaza ratiba ya michuano ya Kombe la Kagame itakayoanza kutimua vumbi Julai 18, 2015 jijini Dar es salaam ikishirikisha timu 13 kutoka nchi wanachama wa CECAFA.

Mechi ya ufunguzi tarehe 18 Julai, 2015 Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam itashuhudiwa wakati wenyeji Yanga SC wataminyana na Gor Mahia ya Kenya, huku APR ya Rwanda ikicheza na Al Shandy ya Sudan na KMKM ya Zanzibar wakifungua dimba na Telecom ya Somalia.

Ratiba ya michuano hiyo imeziweka timu hizo katika makundi matatu ambapo kundi A lina timu za: Yanga (Tanzania), Gor Mahia (Kenya), Telecom (Djbiout), KMKM (Zanzibar) na Khartoum-N (Sudan)

Kundi B: APR (Rwanda), Al Shandy (Sudan), LLB AFC (Burundi) na Heegan FC (Somalia), Kundi C: Azam FC (Tanzania), Malakia (Sudan Kusini), Adama City (Ethiopia) na KCCA (Uganda)

Timu tatu zitakazoshika nafasi ya juu kutoka kundi A, timu mbili za juu kutoka kundi B & C, na mshindi mwenye wastani mzuri kutoka kundi B & C zitaingia katika hatua ya robo fainali.

66 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2015/07/02/cecafa-watoa-ratiba-kagame-2015/">
RSS