TAIFA STARS YAONYESHA MABADILIKO DHIDI YA WENYEJI UGANDA (THE CRANES)

 

TAIFA STARS YAONYESHA MABADILIKO DHIDI YA WENYEJI UGANDA (THE CRANES)

Kikosi cha Taifa Star
Kikosi cha Taifa Star

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premieum Lager imetoka sare ya bao 1- 1 dhidi ya wenyeji Uganda (The Cranes) katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za CHAN mwaka 2017 nchini Rwanda uliofanyika uwanja wa Nakivubo.

John Bocco akishangilia baada ya kuipatia Tanzania bao la kwanza kwa mkwaju wa penati
John Bocco akishangilia baada ya kuipatia Tanzania bao la kwanza kwa mkwaju wa penati

Stars ambayo imeonekana kubadilika katika mchezo wa huo, ilicheza soka la kuvutia tangu mwanzo mpaka mwisho wa mchezo hali iliyowaacha midomo wazi  wenyeji Uganda.

Mpaka dakika 45 za mchezo  kipindi cha kwanza zinamalizika bila kufungana. Kipindi cha pili kilianza kwa Stars kufanya mashambulizi mfululizo kupitia kwa washambuliaji wake John bocco na Rashid Mandawa.

Dakika ya 58, John Bocco aliipatia Tanznaia bao la kwanza kwa mkwaju wa penati kufuatia mlinzi wa Uganda Bakaki Shafik kuunawa mpira wa ndani ya eneo la hatari.

Mara baada ya bao hilo Uganda walifanya mashambulizi mfululizo katika lango la Stars na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha dakika ya 82, kupitia kwa mchezaji Kizito Hezron.

Rashid Mandawa akimtoka Hassani Maswa
Rashid Mandawa akimtoka Hassani Maswa

Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika Uganda 1 – 1 Tanzania. Kwa matokeo hayo Uganda wanasonga mbele kwa ushindi wa jumla ya mabao 4 – 1 na sasa watakutana na Sudan.
Mara baada ya mchezo huo kocha mkuu wa Taifa Stars, Charles Mkwasa amesema anashukuru vijana wake wamejitahidi kucheza vizuri, mchezo ulikua mzuri timu ilitengeneza nafasi chache na kuweza kutumia nafasi moja iliyopatikana.
Mkwasa amewaomba watanzania kuendelea kuwapa ushirikiano, wamekaa na timu kwa muda mfupi wa wiki moja tu lakini katika mchezo wa jana mabadiliko yameonekana, hivyo wanahitaji muda kidogo kuweza kukaa na vijana kwa muda mrefu ili kujenga timu bora.

Mashabiki wakishangilia
Mashabiki wakishangilia

Taifa stars inatarajiwa kurejea Tanzania siku ya jumatatu mchana kwa usafiri wa shirika la ndege la Rwanda Air.

Taifa Stars: Ally Mustafa, Shomari Kapombe, Haji Mngwali, Nadir Haroub, Kelvin Yondani, Mudathir Yahya, Deus Kaseke, Frank Domayo, Said Ndemla John Bocco, Rashid Mandawa, Salum Telela, Saimon Msuva, Ramadhan Singano.

The Cranes: James Alitho, Muzamiru Mutyaba, Brian Ochwo, Hassan Waswa, Denis Oola, Faruk Miya, John Shemazi, Robert Sentongo, Bakaki Shafik, Tekkwo Derick, Kizito Hezron, Kalanda Frank.

68 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2015/07/06/taifa-stars-yaonyesha-mabadiliko-dhidi-ya-wenyeji-uganda-the-cranes/">
RSS