AZAM FC BINGWA CECAFA KAGAME CUP 2015

Timu ya soka ya Azam Fc ya Tanzania imeutwaa ubingwa kwa kombe la Cecafa kagame Cup kwa mwaka 2015.

Baada ya kuichapa timu ya Gor Mahia ya Kenya kwa mabao 2-0 kwenye mchezo wa fainalia uliofanyika katika uwanja wa taifa Jijini Dar es Salaam Tanzania.

Mabao ya Azam maarufu kama wanalambalamba yalifugwa na washambuliaji wake John Bocco na Kipre Tchetche aliyepiga mpira wa adhabu nakuzama moja kwa moja nyavuni.

Wanalamba lamba hao wametwaa uchampion huu wa kwanza bila ya nyavu zake kutikiswa.

Katika mchezo wa awali KCCA ya Uganda iliichapa Al Khartoum 2-1 na kutwaa nafasi ya Mshindi wa 3 wa Kagame Cup.

Kocha Mkuu wa Azam FC, Stewart Hall akiwa amebebwa na wachezaji wa timu hiyo baada ya kumalizika kwa mchezo wa fainali ya Kombe la Kagame dhidi ya For Mahia ya Kenya uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Azam ilishinda 2-0.
Kocha Mkuu wa Azam FC, Stewart Hall akiwa amebebwa na wachezaji wa timu hiyo baada ya kumalizika kwa mchezo wa fainali ya Kombe la Kagame dhidi ya For Mahia ya Kenya uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini
Dar es Salaam. Azam ilishinda 2-0.

Bao za KCCA zilifungwa na Michael Birungi na Muzamir Mutyaba na lile la Al Khartoum kuingizwa na Ousmaila Baba.

Azam FC kwa kuwa Mabingwa wa Kagame Cup wamezoa Kombe pamoja na kitita cha Dola 30,000 huku Gor Mahia wakipata Dola 20,000 na KCCA Dola 10,000

Nahodha wa Azam John Bocco akipokea kitita cha dola za kimarekani dola elfu 30.
Nahodha wa Azam John Bocco akipokea kitita cha dola za kimarekani dola elfu 30.

 

22 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2015/08/03/azam-fc-bingwa-cecafa-kagame-cup-2015/">
RSS