BONDIA LULU KAYAGE AIBUKA MSHINDI AFRIKA YA KUSINI

BONDIA LULU KAYAGE AIBUKA MSHINDI AFRIKA YA KUSINI

BONDIA wa Kike Lulu Kayage mwishoni mwa wiki iliyopita aliibuka kidedea nchini Afrika ya kusini baada ya kumchapa  vibaya   Lizbeth Sivhaga wa nchini humu ukiwa ni mpambano wake wa kwanza  kucheza nje ya nchi na kufanikiwa kushinda kwa T.K.O ya raundi ya pili mchezo huo ulianza kwa kasi ambapo kila mmoja alikuwa na nia ya  kumpiga mwenzie raundi za awali, hata hivyo ilivyofika raundi ya pili bondia Lulu Kayage alimzidi nguvu  mpinzani wake kwa makonde ya mfululizo hadi  wasaidizi wake kumuokoa kwa kumtupia taulo hivyo kusababisha Lulu kushinda T.K.O ya raundi ya pili.

ushindi wa Llulu Kayage ulichagizwa na kocha maarufu nchini Rajabu Mhamila ‘Super D’ ambapo siki mbili kabla ya kuondoka nchini alimzawadia vifaa mbalimbali vya mchezo wa masumbwi na kumhakikishia ushindi kwa asilimia zote.

bondia huyo anatarajia kurudi nchini agost 11 kwa ajili ya maandalizi ya mipambano yake mingine ya kimataifa wakati huo huo bondia Ramadhani Shauri akipoteza mpambano wake kwa kupigwa K.O ya raundi ya nne na bondia mzoefu Philip Ndlovu wa Afrika ya Kusini katika  mpambano wa  raundi nane ulioishia  katika raundi ya nne.

Bondia Lulu Kayage akiwashukuru mashabiki kwa kuwapigia magoti baada ya kumchakaza bondia Lizbeth Sivhaga wa Afrika ya Kusini mwishoni mwa wiki iliyopita
Bondia Lulu Kayage akiwashukuru mashabiki kwa kuwapigia magoti baada ya kumchakaza bondia Lizbeth Sivhaga wa Afrika ya Kusini mwishoni mwa wiki iliyopita

30 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2015/08/10/bondia-lulu-kayage-aibuka-mshindi-afrika-ya-kusini/">
RSS