TAHA WAPATA UONGOZI MPYA

TAHA  WAPATA UONGOZI MPYA

taha

 

Chama cha Mpira wa Mikono Tanzania (TAHA)  jumamosi Agosti 29, 2015 kimefanya uchanguzi  wake uliosimamiwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT)  katika Ukumbi wa Uwanja wa Taifa  baada ya kukamilika kwa Usaili  Agosti 28 Ofisi za Baraza la Michezo.

Katika uchaguzi huo  Chama cha Mpira wa Mikono kimefanikiwa kupata viongozi  wapya  na baadhi waliokuwepo katika uongozi uliomaliza muda wao kurejea tena  katika uongozi huo huku nafasi ya Mweka hazina na Kamisheni ya Ufundi  ikibaki wazi kwa kukosa wagombea.

 

 

Mwenyekiti mpya wa  (TAHA)  Brig. Gen. Julius A. Mbilinyi
Mwenyekiti mpya wa (TAHA) Brig. Gen. Julius A. Mbilinyi

 

Baraza limeuagiza uongozi mpya  kufanya michakato ya uchaguzi mdogo mapema baada ya makabidhiano ya ofisi  ili kupatikana  kwa  wagombea wa nafasi zilizoachwa  wazi kwani ni nafasi muhimu sana kwa maendeleo ya mchezo huo.

Makamu Mwenyekiti wa (TAHA) Michael M. Chibawala
Makamu Mwenyekiti wa (TAHA) Michael M. Chibawala

Nafasi ya Mwenyekiti imenyakuliwa  na  kiongozi na mwanamichezo mzoefu  wa muda  mrefu Brig. Gen. Julius A. Mbilinyi na Makamu wake Mwl. Michael M.Chibawala  waliopita kwa kura zote bila kupigwa.

Katibu Mkuu (TAHA) Fortunatus M.K. Nyamhanga
Katibu Mkuu (TAHA) Fortunatus M.K. Nyamhanga

Nafasi zingine katika uongozi mpya wa Chama cha Mpira wa (TAHA) ni nafasi ya Mwenyekiti Kamisheni ya Ufukweni iliyochukuliwa na Patrick Kahwa kura 17,  Mwenyekiti  Kamisheni ya Tiba Juma Mbawala  mwenye kura 17  na Mwenyekiti Kamisheni ya Sheria na Uamuzi iliyochkuliwa na Waziri Lwimbo kwa kura 16.

taha6
Katibu Mkuu Msaidizi (TAHA) Ruth Kiwia

Wajumbe katika Uongozi mpya wa (TAHA) ni Moshi Bitege aliyeibuka kwa kura 12, Beatrice Mutsinzi na Joseph Mhagama  waliofungana kwa kura 10 kila mmoja.

 

298 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email4
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2015/09/01/taha-wapata-uongozi-mpya/">
RSS