TIMU SITA ZAWAKILISHA “ALL AFRICAN GAMES”

TIMU SITA ZAWAKILISHA “ALL AFRICAN GAMES”

tff

Tanzania inawakilishwa na timu sita  katika Michezo ya Afrika nchini Congo Brazaville ijulikanayo kama “All African Games”, michezo itakayofunguliwa rasmi tarehe 4 Septemba, 2015.  Timu zinazoiwakilisha ni Ngumi, Mpira wa Miguu kwa Wanawake, Kuogelea,  Walemavu, Riadha na Judo.

Timu zitaondoka kwa awamu tatu ambapo Wanamasubwi  wameondoka  jumapili tarehe  30 Agosti, 2015 ikiwa na wachezaji  watatu (3) na kiongozi mmoja  ambao mchezo wao  utaanza  tarehe 2 Septemba  na kumaliza mzunguko wao  Septemba  11.  Wachezaji wa ngumi  wameambatana  na  Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT)  Bwana Henry Lihaya.

ngum

 

Kundi la pili lenye timu mbili linaondoka leo tarehe 1 Septemba, ambapo itakuwepo timu ya mpira  wa miguu wanawake yenye jumla ya watu 23 pamoja na Viongozi  ambapo mchezo wao wa kwanza utakuwa siku ya ufunguzi wa mashindano hayo tarehe 4 septemba na kumaliza mzunguko  septemba  18. Timu ya pili inayoongozana nayo ni timu ya kuogelewa  yenye wachezaji wawili na kiongozi mmoja ambayo itacheza tarehe 6 na kumaliza michezo yake septemba 11.

paralimpiki

Ambapo kundi la mwisho litaondoka Septemba  11 na jumla ya timu tatu ambazo ni timu ya Walemavu, Riadha na Judo ikiwa na jumla ya watu kumi  wakati timu zote tatu zitaanza michezo yao  Septemba  13.  Mashindano hayo yanatarajiwa kuhitimishwa Septemba  19 na wachezaji wa Tanzania wanatarajia kurejea  tarehe 20 mwezi huu.

judo

Tuna imani timu zitatuwakilisha vyema  Watanzania kwa pamoja  tuziunge mkono  na tuzidi kuziombea.

41 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2015/09/01/timu-sita-zawakilisha-all-african-games/">
RSS