KATIBA YA CHAKUTA YATAKIWA KUREKEBISHWA

KATIBA YA CHAKUTA YATAKIWA KUREKEBISHWA

Mwenyekiti mpya wa Chama cha Kuogelea Tanzania (CHAKUTA) mwenye mkoba , Alex Moshi akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wapya wa chama hicho mara baada ya kuchanguliwa katika uchaguzi wa kitaifa wa chama hicho tarehe 10 Oktoba, 2015, mjini Morogoro.
Mwenyekiti mpya wa Chama cha Kuogelea Tanzania (CHAKUTA) mwenye mkoba , Alex Moshi akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wapya wa chama hicho mara baada ya kuchanguliwa katika uchaguzi wa kitaifa wa chama hicho tarehe 10 Oktoba, 2015, mjini Morogoro.

Chama cha kuogelea Tanzania (CHAKUTA) kimetakiwa kurekebisha Katiba ya chama hicho ambayo ilipitishwa tangu mwaka 2006, kutokana na kutokuwa na vigezo vinavyokidhi kasi ya ukuaji wa mchezo huo nchini pamoja na kutokuwa na uwezo wa kukabiliana na changamoto za mchezo huo.

Akiongea wakati wa uchanguzi wa Kitaifa wa kuchagua viongozi wapya wa Chama hicho tarehe 10 Oktoba, mjini Morogoro, Msajili wa Vyama vya Michezo, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Allen Alex alifafanua kuwa katiba ndio inayotoa  mamlaka ya utekelezaji wa shughuli za msingi za kuendeleza mchezo wa uogeleaji nchini, lakini pia  kutokuwa na katiba bora kwa chama hicho kunapunguza kasi ya juhudi za chama hicho kuweza kushirikiana na serikali kutekeleza shughuli za kuuendelezaji mchezo huo.

“Unapokuwa na katiba ambayo haiwaruhusu wawakilishi wa mchezo huo kutoka Zanzibar kuchagua viongozi wa CHAKUTA, suala  hili linaweza kupunguza uwajibikaji wa viongozi hao kwa wanachama ambao hawajawachagua, vilevile wanachama hao wanashindwa kuwawajibisha viongozi ambao hawafanyi juhudi za kuendeleza mchezo huo. Katiba bora ya chama ndiyo inayowezesha usimamizi  mzuri  na uhamasishaji wa   wa michezo unafanywa na serikali” alisema Allen.

Aliongeza kuwa rasilimali fedha ni muhimu sana katika kuendeleza mchezo huo lakini katiba ya sasa haitambui nafasi ya Mkurugenzi wa Fedha ambaye kimsingi ndiye msimamizi wa  fedha za kuendeleza mchezo huo, lakini kutotambuliwa kwa Mkurugenzi huyo kikatiba kama viongozi wengine ambao ni mwenyekiti, katibu  Mkuu na Mweka Hazina kunapunguza ufanisi wa shughuli za uendelezaji wa mchezo.

Msajili wa vyama vya Michezo Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Allen Alex akitoa maelakezo kwa Viongozi wapya (hawapo pichani) baada ya Uchaguzi kumalizika mjini Morogoro mwishoni mwa wiki.
Msajili wa vyama vya Michezo Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Allen Alex akitoa maelakezo kwa Viongozi wapya (hawapo pichani) baada ya Uchaguzi kumalizika mjini Morogoro mwishoni mwa wiki.

Alex alibainisha kuwa marekebisho ya Katiba ya chama hicho yaende sambaba ya uanzishwaji wa vyama vya kuogelea vya Mikoa na Vilabu Wilayani ili kuweza kudumisha uhai wa chama hicho kuanzia ngazi ya Mkoa pamoja na kuendeleza mchezo huo  kukuwa kwa kasi  kubwa.

“CHAKUTA kimekuwa kinatumia vilabu vya kuogelea vilivyopo katika ngazi ya mikoa badala ya kuwa na angalau  vyama vya mikoa 15  vya mchezo huo ili kuwa na uwezo wa kuanzisha chama cha kitaifa. Kutokuwepo kwa vyama vya mikoa kutapunguza kasi ya utekelezaji wa katiba bora ambayo mtairekebisha.” Alisema alex

Akiongea mara baada ya kuchaguliwa, Mwenyekiti mpya wa chama hicho, Alex Moshi alilishukuru Baraza la Michezo la Taifa kwa ushirikiano ambao limekuwa likiutoa kwa chama hicho katika kuendeleza na kuhamasisha mchezo huo nchini.

“Tumekuwa tukipata miongozo mizuri ya kuendeleza mchezo wetu kutoka Baraza hili la michezo, naamini kwa katiba bora ambayo itakuwa imefanyiwa mabadiliko tutaweza kuendeleza mchezo huu kuanzia ngazi za mikoa hadi  za kitaifa”  alisema Moshi

Uchaguzi wa Kitaifa wa viongozi wapya wa CHAKUTA, ulisimamiwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) ambapo viongozi  waliochaguliwa watatumika katika nafasi zao kwa kipindi cha miaka minne, katika ngazi ya Mwenyekiti ni; Alex Moshi, Mwenyekiti Msaidizi- Thauriya Diria,  Katibu Mkuu-Ramadhan Namkoveka,  Katibu Mkuu Msaidizi- Sheha Ali, Mweka Hazina – Imani Dominick, Mweka Hazina Msaidizi- Ayoub Nkuzi, Mkurugenzi wa Ufundi-Amina Mfaume,  Mwakilishi CHAKUZA – Mwalim Mwalim, Mkurugenzi wa Fedha-  Philip Saliboko, Mkurugenzi wa Mashule na Vilabu-Salmin Uled na Mkurugenzi wa Mkaundi Maalum- Geofrey Mwakebende.

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Kuogelea Tanzania (CHAKUTA) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wapya wa chama hicho mara baada ya kufanya uchaguzi wa kitaifa wa viongozi wa chama hicho tarehe 10 Oktoba, 2015, mjini Morogoro.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Kuogelea Tanzania (CHAKUTA) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wapya wa chama hicho mara baada ya kufanya uchaguzi wa kitaifa wa viongozi wa chama hicho tarehe 10 Oktoba, 2015, mjini Morogoro.

18 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2015/10/12/katiba-ya-chakuta-yatakiwa-kurekebishwa/">
RSS