CHEKA ULINGONI UINGEREZA NOVEMBA 7

 

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Advance Security Limited, Juma Ndambile (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na bondia Francis Cheka (wa Kwanza kulia) mara baada ya tuzo za Taswa. Wengine katika picha ni mwandishi mkongwe wa habari za michezo nchini, Saidi Salim, Emmanue Mlundwa, Anthony Ruta na Cosmas Cheka.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Advance Security Limited, Juma Ndambile (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na bondia Francis Cheka (wa Kwanza kulia) mara baada ya tuzo za Taswa. Wengine katika picha ni mwandishi mkongwe wa habari za michezo nchini, Saidi Salim, Emmanue Mlundwa, Anthony Ruta na Cosmas Cheka.

Bondia wa ngumi za kulipwa, Francis Cheka atapanda ulingoni mjini Manchester Uingereza Novemba 7 kupambana katika pambano lisilokuwa la ubingwa.

Akizungumza kwa njia ya simu jana, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Advance Security Limited, Juma Ndambile amesema kuwa Cheka anatarajia kuondoka wiki ijayo kwa ajili ya pambano hilo.

Ndambile ambaye ni meneja wa Cheka, alisema kuwa tayari msaidizi wake, Rashid Nassoro yupo nchini Uingereza akiwa na mabondia wengine wawili huku akikamilisha maandalizi ya mwisho ya pambano hilo.

Kwa mujibu wa Ndambile, Cheka anaweza kupambana na mpinzani wake wa awali, Martin Murray au bondia mwingine kutokana na sababu mbalimbali za kiufundi.

 “Maandalizi yanaendelea vizuri na msaidizi wangu, Rashid Nassoro, kwa sasa yupo Uingereza akikamilisha masuala ya pambano hilo, kuna baadhi ya vitu vilikuwa havijakamilika, ila pambano ni Novemba 7 na leo jioni nitajua lini tutaondoka Tanzania,” alisema Ndambile ambaye kwa sasa yupo Kenya kikazi.

Alisema kuwa Cheka kwa sasa yupo mkoani Morogoro akiendelea kujiandaa na pambano hilo na kama unavyojua, akishinda, atapata ofa kubwa katika mchezo wa ngumi za kulipwa.

Alisema kuwa Cheka anatakiwa kushinda pambano hilo ili kusaini mkataba mnono wa zaidi ya dola za Kimarekani 25,000 (Sh milioni 50) ili kupigana katika pambano linalofuata la ubingwa

 “Lengo ni kumfanya bondia bora ili hata akiachana na masumbwi ya kulipwa, awe na maisha mazuri, chini yangu pia nitamfundisha jinsi ya kuwekeza katika biashara na kujipatia kipato, nilisikitishwa sana matatizo aliyopata,” alisema Ndambile.

Alisema kuwa Cheka amekuwa na heshima kubwa hapa nchini na ghafla heshima hiyo kupotea kutokana na mambo ya ‘kidunia’ na yeye ameamua kumkwamua kabisa.

Wakati huo huo; Bondia Benki Mwakalebela ambaye alitakiwa kupanda jukwaani jana usiku, hakuweza kufanya hivyo baada ya pambano lake kuairishwa dakika za mwisho.

Ndambile alisema kuwa Mwakalebela alitakiwa kupambana na bondia Craig Kennedy na pambano hilo limefutwa kutokana na sababu za kiufundi

 

 

226 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by EmailO
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2015/11/03/2124/">
RSS