WANASOKA WANAWAKE ZAIDI YA 400 WASHIRIKI TAMASHA LA LIVE YOUR GOALS

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (katikati mwenye traksuti ya bluu) katika picha ya pamoja na wanasoka wanawake kutoka katika shule 5 za msingi na vilabu 6 vya mpira wa miguu wa wanawake baada ya kuhitimisha tamasha la Live Your Goals lilifanyika jana jijini Dar es Salaam katika Viwanja vya Karume.

Watanzania wametakiwa kuibua vipaji vya michezo hasa mchezo wa mpira wa miguu kwa wanawake kwani michezo ni afya, biashara na ajira inayoheshimika katika jamii.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel jana wakati wa tamasha la Live Your Goals kuhamasisha mpira wa miguu wa wanawake lililoandaliwa na FIFA na kufanyika jana katika viwanja vya Karume Jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wanasoka wanawake kutoka katika vilabu mbalimbali vya mpira wa miguu wakisakata kabumbu jana jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Karume wakati wa tamasha la Live Your Goals kuhamasisha mpira wa miguu wa wanawake lililoandaliwa na FIFA.

Prof Gabriel amesema kuwa wazo la kuboresha michezo nchini linapaswa kuwekewa jitihada katika kila Mkoa kwa kuwa na timu ya mpira wa wanawake ili kuweza kuchuja lulu itakayotengenezwa na mikoa yote nchini hivyo kuinua vipaji vya michezo.

“Kama wazazi wote nchini wataweza kutambua vipaji vya watoto wao, kuviheshimu na kuviendeleza katika fani mbalilmbali ikiwemo michezo Tanzania itakua katika nafasi nzuri katika mashindano mbalimbali ya michezo duniani” alisema Prof. Gabriel.

Akizungumza wakati wa tamasha hilo Naodha wa Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu Wanawake Twiga Stars ambaye pia ni balozi wa tamasha la Live Your Goals Bibi. Sophia Edward amesema kuwa tamasha la Live Your Goals limekua na muitikio mkubwa kwani wasichana wapatao 400 wenye umri kati ya miaka 12 na kuendelea wameshiriki na kupatiwa nafasi ya kuonyesha vipaji vyao katika mchezo wa mpira wa miguu.

Bibi. Edward amesema kuwa tamasha lililofanyika jana katika viwanja vya Karume ni tamasha la pili baada ya kufanya tamasha la kwanza Mkoani Geita mwezi Julai na kuendelea kuhamashisha wanawake wote wenye vipaji nchini kujitokeza wanaposikia tamasha la mpira wa miguu kwa wanawake linafanyika kwani matarajio ya FIFA ni kufikia na kuibua vipaji vya wanawake nchini.

Naye Bibi. Pili Said mzazi wa mwanamke mwanasoka mwenye umri wa miaka 10 amekiri kujaribu kuzima ndoto ya mototo wake mara kadhaa baada ya kumzuia kucheza mpira wa miguu hivyo kuwataka wazazi wote nchini kutafakari na kuheshimu ndoto za vijana wao ili kuweza kutimiza azma zao.

61 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2015/11/28/wanasoka-wanawake-zaidi-ya-400-washiriki-tamasha-la-live-your-goals/">
RSS