Nyerere Cup (TBA) kuanza Desemba 5

Mashindano ya Mchezo wa Vinyoya Tanzania (TBA) kuanza kutimua vumbi jumamosi ya tarehe 5 kuanzia saa 7 mchana mpaka saa 3 usiku na kufikia tamati Desemba 6 kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa tatu usiku.

vnyoya

Mashindano yatahusisha nchi 3, Tanzania ,Kenya na Uganda, yatafanyika katika kumbi 3 tafauti, Shiskunj, Khalsa Sports Club na katika Ukumbi wa Taasisi ya Badmintoni (Badminton Institute) Mtaa wa Kisutu jijini Dar es salaam.

Akitoa ufafanuzi katika Mkutano na Waandishi uliofanyika katika Ukumbi wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) jana tarehe 2 Desemba, Katibu Mkuu wakuteuliwa wa (TBA) Anthony De’souza,“alisema kuwa mashindano hayo yatakuwa ya mwanamke/mwanaume mmoja mmoja (Ladies/ Men single), watu wawili wawili ( Men/ Ladies double) na awamu ingine itakuwa mchanganyiko (mixed).

Awali, Makamu Mwenyekiti Mzee Timothy Kahoho alisema kuwa Oktoba 22 mwaka huu baada ya Baraza la Michezo kuwateua liliwaagiza mambo makuu manne yakufanya ndani ya miezi ya mitatu(3) ya kuitumikia (TBA).

Aliendelea, moja ya maagizo ya Katibu Mkuu wa Baraza ni kufanya mashindano ya mchezo wa Vinyoya ambayo ndiyo tunaanza nayo “ alisema Mzee Kahoho”.

Mengine ni kufanya Uchaguzi Mkuu ili kuwapata Viongozi wa TBA wakudumu, kuhamasisha wanachama wapya katika chama cha mchezo wa vinyoya na agizo la mwisho lakani siyo mwisho kwa umuhimu ni kufuata Katiba ya Chama katika kila tutakalofanya la mchezo huu katika uongozi wetu.

Mzee kahoho alisema, nia yao ni kuhakikisha Mchezo wa vinyoya unarudi katika thamani ya enzi ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu nyerere ambaye aliweza kuufadhili na Mwaasisi wa mchezo huu marehemu Mwalimu Kente na wenzake waliitangaza nchi kimataifa miaka ya 1960.

Aidha katika kuenzi juhudi za Kente, kamati yetu inakusudia mwakani kuanzisha mashindano ya shule za sekondari katika kuwania Kente Cup, “ alisema Kahoho”.

Akimalizia Katibu Mkuu wa (TBA) Anthony De’souza aliomba Kamati ya Olimpiki (Tanzania Olympic Committee) kuwarudisha ili washiriki katika michezo ya Olimpiki kwani wana uhakika wa kufanya vizuri kwa kuwa wana wachezaji wenye viwango vizuri.

vnyoya2

 

 

70 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2015/12/05/nyerere-cup-tba-kuanza-desemba-5/">
RSS