RT: Mikoa inaua riadha

RIADHA Tanzania (RT) imeitupia lawama mikoa kwa kushindwa kuendeleza mchezo huo nchini.

Kaimu Katibu Mkuu wa RT, Ombeni Zavalla alisema katika mashindano ya wazi yaliyofanyika mwishoni mwa wiki kuwa, uhai wa riadha uko mikononi mwa vyama vya mchezo huo vya mikoa na sio taifa.

Alisema kuwa, ili Tanzania irejee katika mafanikio ya riadha iliyopata katika miaka ya nyuma, mikoa haina budi kuendesha mashindano ya mara kwa mara ili kuwaendeleza.

Pia, Zavalla alisema walimu wa shule za msingi na sekondari hawajui sheria za mchezo huo na ndio wanaoharibu wakati wa mashindano yao kwa kung’ang’ania vitu, ambavyo havipo.

Alisema walimu hao wamekuwa wakitumia sheria ambazo hazipo katika mchezo huo na hilo linatokana na kutopata mafunzo ya uhakika ya mchezo huo kutoka katika mikoa husika.

Aidha, akizungumza baada ya mashindano ya wazi kwenye Uwanja wa Taifa, Mwenyekiti wa Taasisi za Filbert Bayi, Bayi aliipongeza Serikali kwa kuwapatia uwanja huo bure kuendeshea mashindano hayo.

Alisema hatua hiyo ya Serikali itasaidia sana kuuendeleza mchezo huo, ambao umeporomoka sana hapa nchini kwa sababu tofauti tofauti.

Zaidi ya wanariadha 90 kwa wanaume na wanawake 23 walishiriki mashindano hayo, ambapo RT imewataka wanariadha wa jinsi zote kujitokeza kwa wingi ili kuinua mchezo huo.

77 total views, 3 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2015/12/06/rt-mikoa-inaua-riadha/">
RSS