Dar Swim Club watamba kutwaa medali Dubai

Kocha wa klabu ya kuogolea ya Dar Swim Club, Michael Livingstone ametamba kuwa waogelaji wake chipukizi watatwaa medali mbalimbali katika mashindano ya kuogelea ya kimataifa ya Dubai yanayojulikana kwa jina la “Hamilton Aquatics Dubai Long Course” yaliyopangwa kuanza Desemba 11.

Akizungumza jijini jana, Livingstone alisema kuwa waogeleaji wote 13 wapo katika morali ya hali ya juu baada ya kupata maandalizi ya miezi miwili.

Livingstone alisema kuwa mashindano hayo ambayo yanashirikisha waogelaji kutoka nchi mbalimbali duniani, mbali ya kusaka medali, pia yatawapa uzoefu wachezaji wao ambao ni bado chipukizi.

Alisema kuwa mashindano hayo ni makubwa sana katika mchezo huo na hivyo watatumia fursa ili kuwapa uzoefu wa kimatafa waogelaji wao ambao ni hazina ya Tanzania katika mashindano ya kimataifa katika miaka ijayo.
“Timu yetu inaundwa na waogeleaji chipukizi sana, wengi wao chini ya miaka 15, mbali ya kushindana, pia watakuwa wanapata uzoefu wa kimataifa kwa ajili ya kuiwakilisha nchi katika mashindano mengine ya kimataifa kama, Mashindano ya Dunia, Jumuiya ya Madola na michezo ya Olimpiki,” alisema Livingstone.

Alisema kuwa waogeleaji wamesema kuwa hakuna cha kuogopa katika mashindano hayo ambayo yatamalizika Desemba 12, Livingstone.

Kocha mwingine wa timu hiyo, Ferick Kalengela alisema kuwa pamoja na kujiandaa katika katika bwawa la kuogelea la mita 25, wataweza kushindana katika Bwawa la Mita 50 kwani waliongeza muda na umbali wakati wa mashindano.

Kalengela alisema kuwa wamejifunza stamina, kasi ya kuogelea na mambo mengine mengi yanayohusu mashindano hayo na kupata majina ya waogeleaji bora 13.

Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Inviolata Itatiro alisema kuwa maandalizi yote ya safari hiyo yamekamilika na wanatarajia kuondoka nchini kesho Jumatano kuelekea kwenye mashindano hayo.

Inviolata aliwataja waogeleaji hayo kuwa ni Lidia Janik, Deeptti Venugopal, Maia Tumiotto, Ursula Khimji, Anna-Clara Azzoni, Maya Somaiya and Niki Somaiya. Also in the list are Smriti Gokarn, Anjani Taylor, Kayla Temba, Celina Itatiro, Peter Itatiro na Marin de Villard.

Viongozi ni Michael Livingstone na Kanis Mabena ambao ni makocha na Inviolata ambaye ni meneja na mkuu wa msafara.

27 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2015/12/08/dar-swim-club-watamba-kutwaa-medali-dubai/">
RSS