KAMISHENI YA WACHEZAJI TANZANIA (KAWATA)YAFANYA MKUTANO MKUU WA MWAKA

Kamati ya Olimpiki Tanzania  (TOC)  wamewataka Viongozi  wa Mashirika ya  Vyama  vya Michezo  Tanzania  kusaidiana na wanamichezo mbalimbali ili kufikia hadhi ya kimataifa .

Mgeni Rasmi Jamal Nassor Adi akizungumza na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa kamisheni ya Wachezaji Tanzania (KAWATA) katika Ukumbi wa Kituo cha Utengamano Welezo Mjini Zanzibar.
Mgeni Rasmi Jamal Nassor Adi akizungumza na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa kamisheni ya Wachezaji Tanzania (KAWATA) katika Ukumbi wa Kituo cha Utengamano Welezo Mjini Zanzibar.

Hayo yameelezwa na na Katibu mtendaji wa TOC Jamal  Nassor Adi  huko Kituo cha Utengamano Welezo  Zanzibar  wakati alipokua akifungua  Mkutano  mkuu wa mwaka wa Kamisheni ya Wachezaji Tanzania .

Amesema lengo kuu la mkutano huo ni kuhamasisha na kuamsha ari kwa Wachezaji ili kuweza kurejesha hadhi ya Michezo  Tanzania.

Katibu Jamal amefahamisha kuwa wachezaji  ndio wahusika wakuu  wa michezo hivyo ni lazima kushirikishwa na kupatiwa elimu ili kuweza kufahamu  wajibu wao katika michezo   na kuepusha migogoro isiyokuwa ya lazima.

Washiriki wa Mkutano Mkuu wa Mwaka waliohudhuria katika Mkutano huo wakisikiliza maelezo kwa Mgeni Rasmi Katibu Mkuu msaidizi Jamali Nassor Adi (hayupo pichani)
Washiriki wa Mkutano Mkuu wa Mwaka waliohudhuria katika Mkutano huo wakisikiliza maelezo kwa Mgeni Rasmi Katibu Mkuu msaidizi Jamali Nassor Adi (hayupo pichani)

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Akizungumzia suala la dawa za kuongeza nguvu kwa wanamichezo,  Katibu Jamal amesema  ni vyema wachezaji kuzifahamu na kujiepusha nazo kwani kitendo hicho kinaweza kupelekea nchi kupigwa marufuku kushiriki michezo ya Kimataifa.

Nae Katibu wa Kamati ya Olimpiki ya Tanzania Filbert Bayi  amesema kuwa michezo ni chanzo cha kujipatia  ajira  kwa vijana  hivyo ni vyema michezo  iendelezwe ili kuleta maendeleo kwa wachezaji wenyewe  na Taifa kwa ujumla.

Aidha  amesema katika kuimarisha michezo Nchini   suala la   kuteuliwa wawakilishi  wenye uwezo   ni jambo muhimu  na amewashauri washiriki wa mkutano  huo kusaidia ili kupunguza malalamiko.

Mwenyekiti wa  Kamsheni ya  Wachezaji Tanzania (KAWATA)   Ramadhani Zimbwe ameahidi kupambana na rushwa kwa viongozi na watendaji  wa michezo nchini kwani  vitendo hivyo vinarudisha nyuma  ufanisi wa michezo.

Amesema rushwa ni adui wa haki na mara nyingi hupelekea mtu mwenye uwezo wa kifedha kupata haki asiyostahiki na kumuacha mwenye haki hiyo kuikosa kutokana na kukosa fedha.

Wajumbe wakiwa katika picha ya Pamoja.
Wajumbe wakiwa katika picha ya Pamoja.

202 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email5
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2015/12/11/kamisheni-ya-wachezaji-tanzania-kawatayafanya-mkutano-mkuu-wa-mwaka/">
RSS