WAOGELEAJI TANZANIA WANG’ARA

Timu ya Taifa ya mchezo wa kuogelea imetwaa medali 45 katika michuano ya Afrika iliyoanza tarehe 11 na kumalizika 13 mwaka huu nchini Uganda.

Timu ya Tanzania wakiwa na medali walizopewa baada ya kushika nafasi ya pili.
Timu ya Tanzania wakiwa na medali walizopewa baada ya kushika nafasi ya pili.

Katika mashindano hayo timu ya Tanzania ilijinyakulia medali 12 za dhahabu, 22 za fedha na 11 za shaba huku kikosi hicho kikikamata nafasi ya nne katika matokeo ya jumla. Waogeleaji waliotwaa medali za dhahabu ni Emma Imhofff aliyeibuka kinara katika mtindo wa ‘breast stroke’ mita 50, Josephine Oosterhuis katika mtindo wa ‘ back stroke’ mita 50.

Waogeleaji wa Tanzania wakiwa na medali za silver
Waogeleaji wa Tanzania wakiwa na medali za silver

Wengine ni Isam Sepetu aliyeng’ara katika mtindo wa ‘backstroke mita 100 na Sonia Tumiotto katika ‘ free style’ mita 50.

Katibu Mkuu (TSA) na kocha wa Timu ya Tanzania ya kuogelea Ramadhan Namkoveka akiwa ameshika saa tayari kwa mchezo kuanza
Katibu Mkuu (TSA) na kocha wa Timu ya Tanzania ya kuogelea Ramadhan Namkoveka akiwa ameshika saa tayari kwa mchezo kuanza

Katibu wa chama cha kuogelea nchini (TSA) Ramadhan Namkoveka alisema wao mbali na ushindi pia wamefanikiwa upinzani mkali kwa waogeleaji hasa kutoka Afrika ya kusini ambao wamekuwa wakiwaburuta sana miaka ya nyuma timu ya Tanzania.

Mchezaji bora wa kike Josephine Oosterhuis miaka 13-14 akiwa na furaha baada ya kukabidhiwa medali zake.
Mchezaji bora wa kike Josephine Oosterhuis miaka 13-14 akiwa na furaha baada ya kukabidhiwa medali zake.

Huu ni mwanzo mzuri kwa waogeleaji wetu, hasa katika kipindi hiki ambacho timu inatafuta tiketi ya mashindano ya Olimpiki, “alisema Namkoveka”.

44 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2015/12/14/waogeleaj-tanzania-wangara/">
RSS