Uhamiaji Malkia wa kombe la muungano

Timu ya Uhamiaji ya mpira wa pete imeibuka kidedea katika shindano la muungano lilifanyika Uwanja wa Gymkhana mjini Zanzibar kuanzia Desemba 15 na kumalizika mwanzoni mwa wiki hii kwa kuzikutanisha Uhamiaji na timu ya JKU katika fainali, huku Uhamiaji wakitetea ushindi wao kwa kuwachapa JKU bao 38 – 25.

Wapenzi wa mchezo wa Netiboli Zanzibar wakifuatilia mchezo huo wa Ligi Kuu ya Muungano kati ya Uhamiaji na JKU uliofanyika uwanja wa Gmykhana Zanzibar.
Wapenzi wa mchezo wa Netiboli Zanzibar wakifuatilia mchezo huo wa Ligi Kuu ya Muungano kati ya Uhamiaji na JKU uliofanyika uwanja wa Gmykhana Zanzibar

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 
Shindano hilo limehusisha timu za Tanzania Bara na visiwani huku timu ya Jeshi Stars ikijitoa kushiriki mashindano hayo ya Muungano katika hatua za mwisho

Timu zilizoshiriki mashindano hayo kutoka Tanzania Bara ni pamoja na mabingwa Uhamiaji, JKT Mbweni, Polisi, Tumbaku ya Morogoro, Mbeya City ya Mbeya.

 Mchezaji wa Timu ya JKU Rose Israel (WA) na Uhamiaji Sofia Komba (C) wakiwania mpira wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Muungano iliofanyika katika uwanja wa Gmykhana Zanzibar Timu ya Uhamiaji imeshinda kwa mabao 38–25.
Mchezaji wa Timu ya JKU Rose Israel (WA) na Uhamiaji Sofia Komba (C) wakiwania mpira wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Muungano iliofanyika katika uwanja wa Gmykhana Zanzibar Timu ya Uhamiaji imeshinda kwa mabao 38–25.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Huku Zanzibar ikiwakilishwa na JKU, Mafunzo, KBZ, Zimamoto, Chake Stars na Wete Stars.

322 total views, 38 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2015/12/22/uhamiaji-malkia-wa-kombe-la-muungano/">
RSS