MIAKA 52 YA MAPINDUZI RUFIJI

 

Chama cha michezo ya jadi Tanzania (CHAMIJATA) Januari 12, 2016, kinatarajia kuadhimisha miaka ya 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa Tamasha la michezo ya Jadi kijiji cha Bungu, Rufiji.

Katika mazungumzo ya simu leo asubuhi na Afisa Habari wa Baraza la Michezo (BMT)Najaha Bakari , Mwenyekiti wa CHAMIJATA Mzee Kazingumbe, alisema, wamepata ufadhili kutoka kwa ‘Matimira Agri Marketing Services (MAMS) katika Tamasha hilo.
Aliongeza kuwa, tamasha litahusisha michezo zaidi ya nane ya jadi ikiwemo, Bao, Mdako, Kukuna nazi, Kulenga shabaha, kusuka ukili, na Mieleka.
Watanzania waendelee kuwekeza katika michezo ili kuitangaza nchi kimataifa, “alisema Kazingumbe.”

14 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2016/01/06/miaka-52-ya-mapinduzi-rufiji/">
RSS