MLAWA AENDELEZA UBINGWA

 

Mchezaji mahiri wa mchezo wa Chess nchini, Hemed Mlawa ameibuka kidedea katika mashindano ya Kombe la Mapinduzi lililofanyika mwanzoni mwa wiki katika Hotel ya Peacock jijini Dar es salaam.

Mlawa aliibuka mshindi wa shindano hilo katika fainali iliyocheza mwanzoni mwa wiki jijini hapa baada ya kuwashinda washiriki zaidi ya 15 wa Kombe hilo.

Mshindi wa kwanza Hemed Mlawa alijishindia kombe na pesa taslimu 300,000/=, huku mshindi wa pili ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama cha Chess Tanzania (TACA) Nurdin Hassuji akijinyakulia medali na pesa taslimu sh. 200,000/=.

Nafasi ya tatu ilichukuliwa na William Kangwa, aliyejipatia zawadi ya sh. 100,00/ na medali, ambapo zawadi hizo zilitolewa na Mgeni Rasmi wa pambano hilo ambaye pia ni Rais wa mfuko wa Chess Tanzania, Vinay Chaudary.

Kiungo mahiri wa zamani wa timu Yanga na mchezaji wa kwanza kucheza soka la kulipwa Ulaya, Sanday Manara ni mmoja ya washindani katika shindano hilo ingawa hakuweza kufua dafu na kuahidi kufanya vizuri zaidi shindano lingine.

Mwezi wa pili Chama cha Chess Tanzania (TACA) wanatarajia kuwa shindano lingine ambapo wamewataka watanzania wafike kwa wingi kujionea.

32 total views, 2 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2016/01/12/mlawa-aendeleza-ubingwa/">
RSS