WAZIRI MKUU ATAKA MASHIRIKISHO NA VYAMA VYA MICHEZO KUMPA MPANGO KAZI

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amevitaka Vyama na mashirikisho ya michezo mbalimbali kumpa mpango kazi wa muda mrefu na mfupi ili kuiwezesha Serikali kushirikiana nao katika kuleta maendeleo ya michezo nchini.

Mhe.Majaliwa ameyasema hayo leo Mjini Dodoma wakati akifunga mashindano ya Hapa Kazi Tu Half Marathon yaliyoanzia katika Chuo cha Biashara (CBE) tawi la Dodoma na kumalizikia katika uwanja wa Jamhuri yenye lengo la kuadhimisha kilele cha Siku 100 za uongozi wa Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt John Pombe Joseph Magufuli tangu aingie madarakani.

“ Serikali ya Awamu ya Tano tumejipanga kuendeleza michezo nchini kwani michezo ni moja kati ya sekta muhimu kwa maendeleo ya wanamichezo na nchi kwa ujumla na pia ni moja ya kujitangaza kimataifa kupitia michezo mbalimbali”alisema Mhe Majaliwa.
Aliongeza kuwa watanzania tufungue shule za michezo yaani ‘Sports Academy’ ambazo zitalenga kukusanya wahitimu wa shule za msingi na sekondari na kuwafundisha sayansi ya michezo ili kuwapa mbinu tofauti za kufaulu kwenye mashindano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa,” alisema Waziri Mkuu
Aidha Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye amesema kupitia wizara yake atajitaidi kuimarisha michezo hasa ukizingatioa Serikali imeweka mkazo katika michezo hivyo yeye kama waziri mwemye dhamana atalisimamia kwa karibu suala la maendeleo ya michezo yote nchini.

“Naahidi kushirikiana na Mashirikisho, vyama na Vilabu vya michezo ili kuimarisha sekta hii kwa kuweka mipango thabiti ya kusimamia na kuiendeleza michezo ili iweze kuleta tija katika jamii ya watanzania”alisema Mhe. Nnauye.

Mbio hizi za Hapa Kazi Tu Half Marathon zimeshirikisha Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Tulia Ackson, baadhi ya mawaziri, wabunge na watu wa rika zote kwa kukimbia umbali wa kilometa 2, kilometa5 na kilometa21 na washindi kupewa zawadi za pikipiki, mabati na fedha taslimu.

Mashindano haya ya hapa kazi Half Marathon yaliyoandaliwa na Chama cha Riadha Tanzania na kudhaminiwa na kampuni ya GSM, TANAPA, Kilimanjaro International Airport,East Teanders, CRDB Bank na DSTV yameandaliwa kwa nia ya kuandaa timu ya Riadha Tanzania kujiandaa na mashindano ya Olompiki yatakayofanyika mwaka huu Rio de Janeiro nchini Brazil

25 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2016/01/30/waziri-mkuu-ataka-mashirikisho-na-vyama-vya-michezo-kumpa-mpango-kazi/">
RSS