DAR SWIM CLUB MABINGWA WASHINDA MASHINANO YA KUOGELEA YA TALISS

Timu ya Dar Swim Club (DSC) imeshinda mashindano ya kuogelea ya Taliss baada ya kuzipiku klabu nyingine nane zilizoshiriki katika mashindano hayo yaliyofanyika kwenye bwawa la kuogelea la Shule ya Kimataifa ya Upanga.

Dar Swim Club ilijikusanyia pointi 2,421 katika mashindano hayo yaliyoshirikisha timu za wanawake na wanaume. Katika mashindano hayo, wanawake wa DSC walikusanya jumla ya pointi 1,526 huku wanaume wakijikusanyia pointi 895 kushinda nafasi ya kwanza katika mashindano hayo yaliyokuwa na ushindani mkubwa.

swim2

Waogelaji wa kike Smriti Gokarn, Celina Itatiro na Maia Tumiotto walichangia zaidi ushindi wa timu hiyo kwa kukusanya pointi nyingi na akwa upande wa wavulana, walikuwa Matt Golembeski, Marin De Villard na Carter Golembeski.

Nafasi ya pili ilinyakuliwa na wenyeji Taliss kwa kupata jumla ya pointi 2,298 huu waogelaji wao wa kiume, Adil Dharmal na Oliver Mclntosh wakiongoza kwa kuchangia pointi nyingi katika ushindi huo.

Nafasi ya tatu ilikwenda kwa Shule ya Kimataifa ya Moshi ambayo ilichanganyika naya Arusha kwa kupata pointi 1,111 huku waogeleaji wake, Josephine Oosterhuis na Pieter De Raadt wakichangia pointi nyingi.

Timu ya kuoglea ya Mwanza ilimaliza katika nafasi ya nne chini ya waogeleaji nyota Elia Imhoff na Emma Imhoff na kufuatiwa ma shule ya kimataifa ya Morogoro chini ya nyota wake, Dennis Mhini na Charlotte Sanford.

swim3

Timu ya Bluefins ilishika nafasi ya sita kwa pointi 553 ambapo waogelaji wake Sahal Harunani alishinda medali ya shaba. Nafasi ya saba ilikwenda kwa timu ya Wahoo iliyokuwa chini ya Ellis Underson na Rania Karume kwa kupata pointi 303 na huku Champions Rise na Kennedy House wakimaliza katika nafasi mbili za mwisho.

Muasisi wa Dar Swim Club Ferick Kalengela alisema kuwa siri kubwa ya ushindi wao ni kujituma na kufanya mazoezi ya kisasa huku Katibu mkuu wa klabu hiyo, Inviolata Itatiro akiwapongeza wachezaji wake na kusema huo ni mwanzo tu na makubwa yatafuatia katika kuendeleza mchezo wa kuogelea nchini.

53 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2016/01/31/dar-swim-club-mabingwa-washinda-mashinano-ya-kuogelea-ya-taliss/">
RSS