MASHINDANO YA FEBRUARI RAPID CHESS YAMALIZIKA

Mashindano ya mchezo wa Chess mwezi wa pili yaliyopewa jina la “February Rapid Chess” yamefikia tamati jana katika ukumbi wa Flamingo Peacock Hotel, Jijini Dar es Salaam.

Nurdin Hassuji ameibuka mshindi wa kwanza katika shindano hilo baada ya kujinyakulia pointi 6.5 akifuatiwa na William Kangwa wa Zambia waliofungana akijinyakulia pointi 6.5 huku alijikuta kuwa mshindi wa pili kutokana na “Bucholz” pointi ndogo kuliko mwenzake

chess2
Kara Louis (aliyeshika tama) akiwa katika mchezo na mchezaji wa zamani wa Yanga na mchezaji wa kwanza kucheza timu za nje Sunday Manara (kulia) katika mashindano hayo.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Huku Kara Louis alimaliza kwa pointi 5.5 na kushika nafasi ya tatu , akifuatiwa na mshindi wa nne Mussa Mangula.

Mashindano hayo ya raundi 8 yalifanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 13 na kumalizika tarehe 14 Februari kwa udhamini wa Tanzania Chess Foundation.

Mwenyekiti wa Chama Cha Chess Tanzania Bw. Geoffrey Mwanyika alisema kuwa chama chake kimejiandaa vizuri kwa ajili ya kueneza mchezo huu unaotumia akili kwa watanzania wengi zaidi.

Awali Mwenyekiti wa Tanzania Chess Foundation ambaye alikuwa mwamuzi wa mchezo huo, amesema yuko tayari kwa ajili ya gharama ya kumleta kocha kwa ajili ya timu ya Taifa ya Tanzania ili waongeze vipaji na kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa

 

 

chess3
Mwenyekiti wa zamani wa chama cha mchezo wa Chess Musa Mangura mshindi wan nne (mwenye miwani) akiwa katika mchezo na mshindi wa pili wa mashindano hayo William Kangwa .

60 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2016/02/15/mashindano-ya-februari-rapid-chess-yamalizika/">
RSS