MHE.MAJALIWA KUKUTANA NA VYAMA VYA MICHEZO.

MHE.MAJALIWA KUKUTANA NA VYAMA VYA MICHEZO.

Waziri Mkuu wa Serikali ya awamu ya tano, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa anatarajia kukutana na Viongozi wa Vyama/Mashirikisho pamoja na wadau wote wa Michezo nchini siku ya jumatano tarehe 17 Februari, mwaka huu saa nane (8) mchana katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Mwenyekiti wa BMT Deoniz Malinzi akifafanua jambo kwa Waandishi (hawapo pichani) wakati wa mkutano nao leo asubuhi katika Ukumbi wa baraza jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa BMT Deoniz Malinzi akifafanua jambo kwa Waandishi (hawapo pichani) wakati wa mkutano nao leo asubuhi katika Ukumbi wa baraza jijini Dar es salaam.

Akizungumza leo asubuhi, Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Deoniz Malinzi, “alisema, Mheshimiwa Waziri Mkuu, atakutana na vyama vya michezo siku hiyo kufuatia ahadi yake aliyoitoa wakati wa mbio za hapa kazi tu zilizofanyika mwishoni mwa mwezi wa kwanza mjini Dodoma.

Aliendelea kuwa lengo la Waziri Mkuu na Mwanamichezo mashuhuri ni kuzungumza na Wizara yenye dhamana, Baraza la michezo la Taifa na viongozi wa Vyama/Mashirikisho na Wadau wa michezo kuhusu hali ya michezo nchini, kuwasikiliza na kupata maoni yao namna Serikali inavyoweza kusaidiana nao kuinua Sekta hii hapa nchini.

Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa Deoniz Malinzi akiwa na Katibu Mkuu wa BMT, Henry Lihaya wakati wa mkutano na Waandishi leo asubuhi.
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa Deoniz Malinzi akiwa na Katibu Mkuu wa BMT, Henry Lihaya wakati wa mkutano na Waandishi leo asubuhi.

Malinzi katika taarifa yake alitoa wito kwa Vyama vya michezo vyote na wadau kufika katika mkutano huo bila kukosa kwani ni fursa na heshima kwa wanamichezo kwa kiongozi wa Serikali kutaka kuzungum,za nao juu ya maendeleo ya michezo nchini.

Alihitimisha kuwa ni vema tukatumia mkutano huo kuieleza Serikali mambo ambayo yangesaidia kuinua Sekta ya michezo nchini

94 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2016/02/16/mhe-majaliwa-kukutana-na-vyama-vya-michezo/">
RSS