MH. MAJALIWA; SERA NA SHERIA YA MAENDELEO YA MICHEZO ZIBORESHWE.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kushirikiana na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kuipitia upya Sera na Sheria ya maendeleo ya michezo nchini ilikupata Sera na Sheria inayoendana na michezo ya wakati wa sasa.

Akizungumza na viongozi wa Vyama, Mashirikisho na Wadau wa michezo nchini kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, tarehe 17 Februari, 2018.Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameiagiza wizara hiyo kuhakikisha mchakato huo unashirikisha Vyama, Mashirikisho na Wadau wa michezo wote nchini.

Baadhi ya Viongozi na wadau wa michezo nchini, Jijini Dar es salaam, wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati alipokutana nao kwenye uwanaja wa Taifa, tarehe 17 Februari, 2016.
Baadhi ya Viongozi na wadau wa michezo nchini, Jijini Dar es salaam, wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati alipokutana nao kwenye uwanaja wa Taifa, tarehe 17 Februari, 2016.

 

“Sera ya michezo imepitwa na wakati kwani ilipitishwa na Bunge mwaka 1967 na kufanyiwa marekebisho mwaka 1971 na sera yake ikachelewa kidogo mpaka mwaka 1995 na ilitungwa sheria kabla ya sera jambo ambalo ni kinyume hivyo naagiza wizara, Baraza la Michezo washirikisheni wadau muandae sera ili baadae itungwe sheria itakayokidhi mahitaji ya michezo nchini”, alisisitiza Majaliwa.

Aliongeza kuwa msingi wa michezo unajengwa na vyama imara vya michezo hivyo kuitaka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kushirikiana na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kuzipitia Katiba za vyama vyote na kuzikagua ili kuhakikisha zinaandaa sera ya michezo inayokwenda na wakati.

“Katiba za vyama vingi vya michezo zinawabebaviongoziwaliopomadarakani, hivyoBaraza la Michezo la Taifa inatakiwa kusimamia na kuondoa neno ridhaa na kuwa ya kulipwa, kwani michezo ni ajira, kwa mfano kwani ni Shirikisho la Soka Tanzania mmeondoa Ofisi ya Chama cha Makocha (TAFCA) ile hali ndio wenye dhamana na kuwasimamia na kuangalia vigezo vya kuajiri makocha hasa wakigeni nchini” alisema Majaliwa.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikagua miundombinu ya Uwanja wa Taifa kabla ya kuongea na Viongozi na wadau wa michezo nchini, kwenye uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam, tarehe 17 Februari, 2016.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikagua miundombinu ya Uwanja wa Taifa kabla ya kuongea na Viongozi na wadau wa michezo nchini, kwenye uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam, tarehe 17 Februari, 2016.

Majaliwa alizitaka Halmashauri nchini kuhakikisha wanaendeleza viwanja vya michezo pamoja na kuvitaka vyama vya michezo kuwa na walimu wa michezo watakaofundisha michezo kisayansi katika matawi ya wilaya ni ili vijana waandaliwe wakiwa wadogo na hatimaye kuwa wanamichezo bora kwa lengo la kuitangaza Tanzania nje ya nchi.
“Tunaelewa ili kupata wananmichezo bora kuna hitajika viwanja bora. Serikali tunaelewa kilio cha vyama mbalimbali vya michezo ambavyo hutumia Uwanja wa ndani wa Taifa, kuna mwekezaji amepatikana ambaye ni Kampuni ya Billion Group, anataka kufanya uwekezaji eneo lile kwa kujenga viwanja vya kisasa hapo. Naiagiza wizara kufanya mawasiliano naye ili aanze uwekezaji huo.”Alifafanua Majaliwa.

MAJALIWA3

Wakati huo huo ameliagiza Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kurudisha mfumo wa tiketi za kielektroni na kuachana na huu wa vitabu ili kupata suluhisho la kudumu la upotevu wa fedha za viingilio viwanjani.

“Ni jambo lililo wazi kuwa tukianza kutumia mfumo huu wa kielektroni kimapato kupitia mchezo wa mpira wa miguu yataongezeka kama mlikuwa mna pata milioni 200 inawezekana ikapanda hadi milioni 300, tamko letu kama serikali ni kuwa hatuta ruhusu utaratibu wa tiketi za vitabu huu unaotumika sasa na badala yake utumike mfumo huo ambao ni salama na una uwazi katika uendeshaji wake” Alisema WaziriMkuu.

Mkutano huo ulioratibiwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT), kufuatia agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kumuagiza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuandaa kikao cha haraka na viongozi wa vyama vya michezo nchini ili wamuelekeze kila mmoja amejipanga vipi kuinua viwango vya michezo katika chama chake, wakati akizungumza na mamia ya viongozi na wakazi mkoa wa Dodoma tarehe, 30, Januari 2016, ambao walishiriki mashindano ya mbio za nusu marathon (km. 21 na km. 5) Mashindano hayo yalijulikana kama “HAPA KAZI TU HALF MARATHON”.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuongea na Viongozi na wadau wa michezo nchini, kwenye uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam, tarehe 17 Februari, 2016.

117 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2016/02/18/mh-majaliwa-sera-na-sheria-ya-maendeleo-ya-michezo-ziboreshwe/">
RSS