BMT IMEMTEUA BWANA MOHAMEDI KIGANJA KUWA KATIBU MTENDAJI.

Baraza la Michezo la Taifa (BMT) limemteua Bwana Mohamed Said Kiganja Kuwa Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza hilo kuanzia leo, ili kujanza nafasi ya aliyekuwa Katibu Mtendaji ambaye amehamishiwa Wizarani na Mheshimiwa Nape Nnauye ili aweze kupangiwa majukumu mengini.

Uteuzi huu ni kwa mujibu wa sheria ya BMT namba 12 ya 1967 kifungu namba 5(1) ambacho kinampa mamlaka Mwenyekiti wa Baraza kumteua Katibu Mtendaji baada ya kupata idhini ya Waziri mwenye dhamana.

Kabla ya uteuzi huo Bwana Kiganja alikuwa ni Afisa Michezo Mkuu katika Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuanzia mwaka 2015 mpaka uteuzi wake ulipofanyika.

Hata hivyo, Bwana Kiganja aliwahi kufanya kazi kama Afisa mwandamizi michezo Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na Afisa Michezo Mkuu katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Bwana Mohamed Kiganja ana shahada ya kwanza ya Elimu katika masuala ya Michezo na Utamaduni kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam.

'Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bw. Dioniz Malinzi (kulia) akimkabidhi ofisi Katibu Mkuu mpya wa Baraza hilo Bw. Mohamed Kiganja mara baada ya kuripoti ofisini hapo kufuatia uteuzi wake kumtaka kuanza kazi leo jijini Dar es Salaam.'
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bw. Dioniz Malinzi (kulia) akimkabidhi ofisi Katibu Mkuu mpya wa Baraza hilo Bw. Mohamed Kiganja mara baada ya kuripoti ofisini hapo kufuatia uteuzi wake kumtaka kuanza kazi leo jijini Dar es Salaam.

99 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2016/02/19/bmt-imemteua-bwana-mohamedi-kiganja-kuwa-katibu-mtendaji/">
RSS