BMT LAANDAA TAMASHA LA MICHEZO SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

 

Baraza la Michezo la Taifa (BMT) limeandaa Tamasha la Michezo kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani litakalofanyika siku ya Jumamosi tarehe 05 Machi, 2016 kabla ya kilele cha siku hiyo Kidunia inayoadhimishwa Machi 08 kila mwaka kuanzia saa 12:30 asubuhi katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam .

Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bw. Dioniz Malinzi (shati jeupe) akifafanua jambo kwa waandishi (hawapo pichani), Makamu Mwenyekiti Zaynab Vulu (mwenye shungi), Kaimu Katibu Mkuu Mohamed Kiganja wa mwisho (kulia) na wa kwanza kulia ni Mjumbe wa Baraza Jeniffer Mmasi Shang'a.
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bw. Dioniz Malinzi (shati jeupe) akifafanua jambo kwa waandishi (hawapo pichani), Makamu Mwenyekiti Zaynab Vulu (mwenye shungi), Kaimu Katibu Mkuu Mohamed Kiganja wa mwisho (kulia) na wa kwanza kulia ni Mjumbe wa Baraza Jeniffer Mmasi Shang’a.

Akizungumzia Tamasha hilo leo asubuhi, Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mhe. Zaynab Matitu Vulu (MB) alieleza kuwa, Baraza kama mdau mkubwa wa Maendeleo ya Michezo, Kijamii , Kiutamaduni na Kiuchumi litashiriki katika maadhimisho ya siku Wanawake Duniani kwa kuandaa shughuli mbalimbali za Kimichezo kwa Wasichana na Wanawake wa rika zote.

Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kushiriki katika siku ya Wanawake Duniani, tunaahidi kuendelea kuadhimisha siku hii kila mwaka, “alisema Mhe. Matitu”.
Aliendelea kusema kuwa, lengo la maadhimisho haya ni kutekeleza majukumu ya Baraza kwa vitendo, Ilani ya Chama cha Mapinduzi na malengo ya Millenia kupitia Michezo la kukuza michezo na kuhamashisha ushiriki, pia ni wakati muafaka wa kutambua mchango wa Wanawake katika Maendeleo ya Michezo nchini.

Aidha, Michezo itasaidia kujenga afya pamoja na kujikinga na Magonjwa yasiyo ambukiziwa, Michezo ni ajira vilevile huleta na kujenga mahusiano mazuri kwa jamii, alisisitiza Mhe. Matitu.

bango

Kauli mbiu ni “50 /50 ifikapo 2030 Tuongeze Jitihada”
“Maendeleo ya Mwanamke kupitia Michezo yanawezekana “.

Baraza linatoa wito kwa wanawake wengi kujitokeza kushiriki Tamasha hilo.

Tamasha hilo litashirikisha Michezo mbalimbali ikiwemo mbio za polepole “Jogging” pamoja na baadhi ya Michezo ya asili.

Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.

109 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2016/03/02/bmt-laandaa-tamasha-la-michezo-siku-ya-wanawake-duniani/">
RSS